Eti! mwanafunzi akacha shule kisa penzi la nguruwe
http://habari5.blogspot.com/2014/10/eti-mwanafunzi-akacha-shule-kisa-penzi.html
UNAWEZA kudhani ni Hekaya za Kusadikika! Lakini ni kisa cha kweli kwamba, mama mzazi amemshitaki polisi mwanaye wa kiume ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha pili mwenye umri wa miaka 16 kwa kile anachodai amechoshwa na tabia ya mwanaye ya kufanya mapenzi na nguruwe wao jike mara kwa mara na hata kujikuta akiacha shule.
Amelalamika akidai kuwa kijana huyo amenogewa `penzi’ la mnyama huyo maarufu hapa kama “kitimoto au Noah” kiasi cha kumfanya aache masomo na kuwa mtoro sugu shuleni.
Nguruwe huyo jike inadaiwa anafugwa na familia ya mwanafunzi huyo anayesoma katika shule moja ya umma ya sekondari, Manispaa ya Sumbawanga.
Hayo yamethibitishwa na Mkuu wa Kitengo cha Polisi Jamii mkoani Rukwa, Sixmund Kibassa aliyemweleza mwandishi wa habari hizi jana kuwa, mama mzazi wa mtoto ameripoti tukio hilo katika jeshi polisi.
Kibassa amesifu uamuzi huo, akisema ni mafanikio makubwa yanayotokana na Mpango Shirikishi wa Kitengo hicho wa kurejesha shuleni watoto ambao ni watoro sugu.
Anasema mwanafunzi huyo (jina limehifadhiwa) ni miongoni mwa watoro sugu 70 kutoka shule mbalimbali za msingi na sekondari katika Manispaa ya Sumbawanga waliorejeshwa hivi karibuni kupitia mpango huo shirikishi wa kuwarejesha watoro shuleni unaotekelezwa na Kitengo cha Polisi Jamii mkoani humo.
Kwa mujibu wa Kibassa, wazazi na walezi wenyewe wanafika katika kitengo hicho cha polisi jamii na kuripoto kuhusu watoto wao ambao wamekatiza masomo .
Aliongeza kusema kuwa, wazazi na walezi hao wanafichua ya kwamba watoto wao hao licha ya kutokwenda shuleni, lakini pia nyumbani hawaonekani kwamba baadhi yao wamebainika kutumia muda wao mwingi kunywa pombe vilabuni badala ya kusoma.
“Sasa hivi karibuni ni juzi tu mama mmoja alinifuata na kuniripotia kisa cha mwanae wa kiume anayesoma Kidato cha Pili katika shule moja ya sekondari kwamba licha ya kuwa mtoro sugu shuleni; lakini pia amekuwa na tabia chafu ya kufanya mapenzi na nguruwe wao jike mara kwa mara …. Nilipomhoji kijana huyo alikiri kufanya hivyo …. basi tulimnasihi, “ alieleza.
Kwa mujibu wa Kibassa baada ya kumsihi mwanafunzi huyo alikubali kuendelea na masomo ambapo alirejeshwa shuleni kwake na kupokelewa na walimu na wanafunzi wenzake kwa furaha.
Daktari wa Tiba ya Binadamu, Dk Paulo Maiga akizungumzia tukio hilo alikiri kuwa mwanadamu kufanya mapenzi na mnyama kuna madhara makubwa ikiwemo kuambukizwa virusi ambavyo vikingia mwilini mwa binadamu kuna uwezekano mkubwa visiweze kutibiwa .
“Hili ni tatizo kubwa madhara yake ni makubwa huyu nguruwe anaweza kuwa ameshambuliwa na virusi vya ugonjwa ambao ukiingia na kumshambulia mwanafunzi huyo upo uwezekanao mkubwa kusiwepo na tiba,“ alisisitiza Dk. Maiga.
Ends