Tuzo za watu 2015 zimekuja kivingine, pendekeza sasa umtakae

Nancy na mumewe pamoja na Meya wa Ilala Jery Slaa na mkewe

Washindi wakiwa kwenye picha ya pamoja


Na Mwandishi Wetu
KWA sasa hapa nchini ni misimu ya Tuzo mbalimbali kwa zinazohusiana na sekta ya sanaa kwa ujumla.

Zipo Tuzo za Muziki za Kilimanjaro Tanzania ambazo zimezinduliwa wiki hii na pia kuna Tuzo za Watu.

Tuzo za Watu kwa msimu huu ulizinduliwa rasmi juzi ambapo mashabiki wa muziki na filamu wanapata nafasi ya kuwachagua wadau wawapendao wanaojihusisha na sekta hizo.

Mashabiki hao wanakuwa na wasaha wa kuwachagua wanamuziki, waigizaji pamoja na watangazaji wa vipindi vya Radio na Luninga na wengineo.

Huu ni mwaka wa pili kwa tuzo hizo kufanyika ambapo wananchi wameanza kuzipokea kwa kupiga kura kwa wale wawapendao.

Katika vipengele vinavyoshindaniwa ni pamoja na Mwigizaji wa kiume anayependwa, Mwanamuziki wa kike anayependwa, Mwanamuziki wa kiume anayependwa, Filamu inayopendwa, Video ya Muziki inayopendwa.

Pia mfadhili wa muziki anaependwa, kipindi cha Luninga kinachopendwa, mwongozaji wa video za muziki anaependwa, mtangazaji wa radio anaependwa, kipindi cha radio kinachopendwa na mengineo.
Pia Video ya muziki inayopendwa, kipindi cha Luninga kinachopendwa, Tovuti au blog inayopendwa pamoja na msanii wa mwaka kwa ujumla.

Mkurugenzi Mtendaji, wa kampuni ya Bongo 5 Media Group Limited, Nancy Sumari, anasema kuwa Tuzo hizo zinalenga kuwapatia wasaha wananchi kuonesha mapenzi yao kwa watu mbalimbali wanaojihusisha na sekta za muziki, filamu na utangazaji.

Anasema kuwa Tuzo hizo zinawapatia wasaha wananchi pia kuhusishwa kwenye utendaji wa kila siku wa wadau hao wanaopendekezwa kwa kuwa kwa kuwachagua wanakuwa wamezitukuza kazi zao.
Anasema kuwa ikiwa juzi ndio zimezinduliwa rasmi Tuzo hizo, awamu ya kwanza ya upigaji kura itafungwa April 16  ambapo yatapatikana majina matano kutoka katika kila kipengele kati ya hivyo 14.
Anafafanua kuwa wananchi watatakiwa kuanza kupiga kura kutokana na orodha ya majina hayo matano kwenye kila kipengele yatakayotangazwa.

Pia anaongeza kuwa mnamo April 30 majina matano yatachujuwa tena kufikia majina manne  na kuwa yamebakia majina manne kutoka katika kila kipengele.

"Sasa baada ya hapo itachukua wiki moja tena mbele na kutafanyika tena mchujo utakaobakiza majina matatu kwenye kila kipengele hivyo 14 na pia wananchi watakuwa na jukumu la kuchagua mshindi kutoka katika majina hayo matatu"alisema Nancy.

"Katika watakaochaguliwa kuingia katika hiyo tatu bora wataalikwa kuhudhuria katika fainali ya Tuzo hizo Mei 7"alisema Nancy.

Akizungumzia zawadi kwa washindi wa kila kipengele, Nancy anasema kuwa kila mshindi ataibuka na kitita cha shilingi Milioni Moja pamoja na Tuzo yenye jina lake na zilizonakshiwa kisanii zaidi.
Anaongeza kuwa kuwa  watakaoshindanishwa ni Mtangazaji wa redio anayependwa, Kipindi cha redio kinachopendwa.
   
Akizungumzia kuhusiana na namna ya uoigaji wa kura alisema kuwa kutakuwa na njia mbili ambazo ni kwa kutumia tovuti ya tuzo  ambayo ni www.tuzozetu.com na kwa njia ya ujumbe mfupi wa simu ambapo utaandika neno TZW kwenda namba 15678.

Nancy anasema kuwa kwa mwaka huu wameamua kutoshirikisha kipengele cha wanamichezo na badala yake kimeongezwa kipengele cha mfadhili bora wa muziki.

Pia kuna vipengele vingine kama vile mwongozaji wa filamu anayependwa, tovuti/blogu inayopendwa na mfadhili maarufu anayependwa.

Wakati huo huo baadhi ya wasanii waliozungumza na gazeti hili wanasema kuwa kuanzishwa kwa tuzo hizo ni mwanya mwengine wa wasanii kuutumia katika kutangaza kazi zao za sanaa.

Msanii wa Muziki Nuhu Mziwanda anasema kuwa Tuzo hizo kwa mwaka huu anaziona ni kama zimekuja kivingine zaidi kwa kuwa wasanii wameongezewa mwanya mkubwa zaidi wa kuwania tuzo hizo.

Anaongeza kuwa Tuzo nyingi zimekuwa zikitumika kuwainua wasanii kwa kuwa wakishinda huzitumia tuzo hizo katika kurasa zao za mitandao ya kijamii ambapo wasanii hao wanajitangaza zaidi na Tuzo zao.

"Kwa mimi naona kuwa ni kama fursa nyingine kwa wasanii hawa kujitangaza zaidi kwa kuwa iwapo wakiwa wamefanya vema wanaweza kushinda tuzo hizo kwa kuchaguliwa na watu ambao kimsingi ndio mashabiki wao, hivyo unaweza kuona ni kwa kiasi gani kama msanii akifanya vema anavyoweza kufahamika zaidi na hicho ndo kipimo chenyewe" alisema msanii huyo.

Kwa upande wake mdau mahiri wa muziki nchini ambae ni Mwanzilishi wa Bendi ya Yamoto, Said Fela anasema kuwa mwaka huu kumekuwa na maendeleo makubwa katika sekta ya sanaa hapa nchini na yanatakiwa kuenziwa.

Anaongeza kuwa kwa kuwepo kwa tuzo zaidi kama Tuzo za Watu ni inshara kuwa kazi sasa za sanaa zinaanza kutambulika zaidi na zaidi.

Pia mwanamuziki wa muziki wa Hip Hop Joe Makini anasema kuwa "Sisi kama wadau wa sanaa hii kwa hapa nchini tunaona kuwa ni vema hata kukawa na hafla nyingi zaidi za utoaji wa Tuzo za Wasanii ili wasanii wawe na wigo mkubwa zaidi wa kujitanua".

Akizungumzia kwa undani zaidi kuhusiana na Tuzo hizo, Mhariri Mkuu wa Gazeti Tando (bloga) ya Bongo5, Fredrick Bundala anasema kuwa Tuzo
“Kwenye jamii yetu kuna watu maarufu ambao wamekuwa mstari wa mbele kusaidia jamii hususan watu wasio na uwezo ama wanaoshi katika mazingira magumu. Tumeona ni muhimu pia kuwatambua watu hawa ambao huamua kujinyima na kugawana kile wanachokipata ili kuwasaidia watu wanaohitaji msaada,” ameongeza.

Anasema kuwa ili kuwapatia mwanya zaidi wananchi  kupendekeza majina ya watu hao wawapendao anasema kuwa mbali na kupiga kura kupitia tovuti pia wanaweza kutumia njia ya ujumbe mfupi wa simu kwa kuandika neno TZW, code ya kila kipengele na jina la anayependekezwa kwenda 15678.

“Baada ya wiki tatu kuanzia leo tutatangaza majina ya washiriki watano waliochaguliwa kuingia kwenye awamu ya kwanza ya mchujo ambapo katika kipindi cha wiki mbili itafanyika michujo mingine miwili ili kuwapata washiriki watatu watakaoingia fainali,” amesisitiza Bundala.
“Washiriki watatu kwenye kila kipengele watahudhuria kilele cha tuzo hizo kitakachofanyika katikati ya mwezi wa tano.”

 “Kura za wananchi ndizo zitakazompata mshindi. Ni muhimu wananchi kuwapigia kura watu wanaowapenda ili kuhakikisha wanashinda vipengele walivyotajwa kuwania,” amesema Mpanda.
Mpanda amevitaja vipengele vinavyowaniwa kwenye tuzo za mwaka huu kuwa ni pamoja na Mtangazaji wa redio anayependwa (TZW1), Kipindi cha redio kinachopendwa (TZW2), Mtangazaji wa kipindi cha runinga anayependwa (TZW3), Kipindi cha runinga kinachopendwa (TZW4), Tovuti/Blogu inayopendwa (TZW5) na Muongozaji wa video za Muziki anayependwa (TZW6).
Vingine ni Muongozaji filamu anayependwa (TZW7), Mwigizaji wa kike anayependwa (TZW8), Mwigizaji wa kiume anayependwa (TZW9), Mwanamuziki wa kike anayependwa (TZW10), Mwanamuziki wa kiume anayependwa (TZW11), Filamu inayopendwa (TZW12), Video ya Muziki inayopendwa (TZW13) na Mfadhili maarufu (TZW14).
Hashtag za kwenye mitandao ya kijamii mwaka huu ni #TZW2015 na #TuzozaWatu.
================

Related

Sticky 6608660007034367294

Post a Comment

emo-but-icon

item