Hennessy yasherekea Miaka 250 ya utaalamu na ubora wa kipekee Dar

Muda umefika wa Hennessy kusherehekea hatua nyingine katika historia yao: adhimisho la miaka 250. Hennessy walisherehekea kufikisha miaka 250 jijini Dar-es-salaam kwa kufanya dinner pale Hyatt Regency jumatano iliopita, huku wakialika mastaa wa Tanzania kutoka nyanzo mbali mbali kama mitindo, vyombo vya habari na wafanya biashara wakubwa Tanzania. Kwa kuwa maadhimisho haya ya miaka 250 yatakuwa yakifanyika duniani kote, balozi wa kimataifa wa Hennessy, Bwana Cyrille Auriol, alisafiri kutoka Ufaransa kuja Dar ili kukutana na wateja waaminifu wa Hennessy pamoja na kuwaelimisha ili kuongeza mwamko wa bidhaa ya Hennessy Tanzania. Wageni walialikwa kuja kujionea pamoja na kujionjea toleo hili la kipekee la Hennessy 250 Collector Blend, kuna chupa chache tu za toleo hili zilizotengenezwa. Chupa hizi ambazo zimetengezwa kipekee kwa ajili ya maadhimisho haya ya mwaka huu na watu wachache wamechaguliwa duniani kote kujaribu kinywaji hichi. Hii ni awamu ya kwanza ya hafla hii ya miaka 250 ya Hennessy ambayo itafanyika katika miezi inayokuja – vitu vikubwa na vizuri zaidi vinakuja kutoka Hennessy. Wakati mwingine utapokuwa unafurahia kinywaji hiki cha Hennessy jiunge na maadhimisho haya kwa kutupia picha kwenye mitandao ukiwa unafurahia Hennessy yako na kuandika #H250TZ na #Hennessy250. Maadhimisho ya Hennessy 250 yanaandaliwa na Qway International , mwakili maalum, waingizaji na wasambazaji wa brand ya Moët-Hennessy Africa Mashariki

Related

Technology 6143908004749338648

Post a Comment

emo-but-icon

item