Wiki ya usalama barabarani yaendelea Moshi
http://habari5.blogspot.com/2017/10/wiki-ya-usalama-barabarani.html
MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan amelitaka jeshi la Polis kuendesha ukaguzi kubaini leseni feki, kisha kuwakamata wahusika wote wanaosaidia uwepo wa lesni za aina hiyo mitaani.
Pia katika kamatakamata hiyo madereva watakaokutwa na leseni hizo wafikishwe kwenye vyombo vya sheria ili kupunguza uwepo wa ajali zitokanazo na uzembe nchini
Samia alitoa agizo hilo jana kwenye uzinduzi wa Wiki ya nenda kwa Usalama barabarani inayoadhimishwa kitaifa mkoani Kilimanjaro ikiwa na kauli mbiu ya Zuia ajali, Tii Sheria na Okoa Maisha.
Alisema, sio kila dereva mwenye leseni anastahili kuwa nayo kwa kuwa ipo idadi kubwa ya madereva wamepata leseni bila ya kuwa na vigezo stahili.
Alisema katika kukamata madereva wa aina hiyo wakague na uhalali wa leseni husika na kasha kukamata zile ambazo sio sahihi.
Alisema, ili kukabiliana na ajali za barabarani nchini kuja haja kubwa ya kuwakabili kwanza madereva wa aina hiyo na kisha kuwachukulia hatua.
Pia amelitaka jeshi la Polis kubuni mbinu za kiteknolojia zitakazosaidia kukamata magari yanayovunja sheria, hilo linaweza kufanyika kiteknolojia bila ya kuwapo kwa askari barabarani.