Lilian Madeje aja na mradi wa kusaidia wakulima kufanya kilimo kiteknolojia akishirikiana na TBL

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Roberto Jarrin akizungumzia nafasi ya TBL katika kuwaendeleza wakulima nchini kiteknolojia ZaidiAdd caption
Mwanzilishi mwenza wa mradi wa Bits and Bytes unaojihusisha na matumizi ya teknolojia na ubunifu, Lilian Madeje, akizungumzia nafasi ya Teknolojia katika kuendeleza kilimo nchini, mradi huo ndio unaoratibu shindano la kuwapata wakulima wanaotumia teknolojia na ubunifu katika kuendeleza kilimo.
Waandishi wa habari wakifuatilia matukio hayo kwa umakini 

Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya Bia nchini(TBL) ambayo ni moja kati ya wanafamilia AB InBev imeandaa shindano linalowahusisha matumizi ya ubunifu na teknolojia kwa wakulima.

Shindano hilo lililozinduliwa jana, litafikia tamati Mei 10 mwaka huu, tukio litakalofanyikia ukumbi wa Mlimani City ambapo washindi watatu watapatikana.

Akizungumza kwenye uzinduzi wa shindano hilo, linalofanyika kwa ushirikiano na Mradi wa masuala ya Teknolojia na Ubunifu Bits & Bytes,  Mkurugenzi Mtendaji wa TBL, Roberto Jarrin, alisema lengo ni kuwatambua na kuwaendeleza wakulima wanaolima kibunifu.

Alisema, kilimo cha kibunifu kinawanufaisha wakulima kwa kuwa wanapata faida ile ile iliyokusudiwa kwa kuwa kinaokoa mazao na mbegu kupotea wakati wa kupanda na wakati wa kuvuna.

“Tanzania Breweries tumeona nafasi ambayo kilimo inayo katika kuendeleza uchumi wa nchi na hilo linaweza kufanikiwa kwa kutumia teknolojia na ubunifu katika kilimo, hivyo shindano hili linalenga kuwafikia wakulima wengi zaidi”alisema Roberto Jarrin.

Kwa upande wake Mwanzilishi mwenza wa Bits and Bytes  Zuweina Farah, alisema katika kuhakikisha kilimo chenye kuhusisha ubunifu na teknolojia unafanikiwa mnamo April 9 watakua SUGECO, na tarehe 10 na 12 watashiriki kwenye kongamano la kilimo biashara mkoani Morogoro.

Aliongeza pia Arusha mnamo April 12 na 13 katika Chuo cha ufundi Arusha kutakuwa na mjadala kuhusiana na kilimo ikiwa pamoja na kutembelea miradi tofauti ya Twende. Huku April 14 hadi 15  itashirikiana na AIESEC kwa Dar na mipango mingine kufanyiwa kazi kufikisha ujumbe kwa wabia tofauti kwenye eneo hili..
=================

Related

Sticky 7899499778598493360

Post a Comment

emo-but-icon

item