Rc Chalamila awafunda wamachinga Mbeya
http://habari5.blogspot.com/2018/12/rc-chalamila-awafunda-wamachinga-mbeya.html
|
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila
Na Mwandishi Wetu, Mbeya
MKUU wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila amewataka
wamachinga mkoani humu kujiendeleza na kuwa wafanyabiashara badala ya kupenda
kuendelea kuwa wamachinga.
Chalamila ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na
HabariLeo kutolea ufafanuzi uamuzi wake wa kuwataka wamachinga waondoke kwenye
maeneo yasiyokuwa rasmi.
Aliwataka wamachinga hao kutambua kuwa umachinga wao
unapaswa kuwa kwa miaka mitatu na zaidi ya hapo wanapaswa kuanza kulipa kodi
zote stahiki.
Alisema.“Kuna mijadala inaendelea kwenye mitandao
ya kijamii kuwa nimewafukuza wamachinga mkoani kwangu sasa swali ni kuwa kama
wao ni wapangaji unawafukuzaje, maana wanasema wamachinga wamefukuzwa,
Ni vema wakafahamu kuwa umachinga haupaswi kuwa sifa
ya kudumu, machinga sahihi inatakiwa uwe mabadiliko ya kuelekea kuwa
mfanyabiashara wa kati katika eneo moja tulivu katika maduka.“
Pia Mkuu huyo wa Mkoa aliitaka ofisi ya Mamlaka ya
Mapato (TRA) mkoani humo kufuatilia ukuaji wa biashara za wamachinga hao ikiwa
ni pamoja na kuwapatia elimu ya maarifa na ujuzi za biashara.
Lakini pia alisisitiza kuwa anawapenda na anata
kuona wananufaika na hivyo katika kutimiza adhma hiyo aliwataka kuwa na Saccos
ya pamoja itakayowasaidia kupata mikopo kwa bei nafuu na hivyo kujipatia faida.
Alisema“Rais Dk John Magufuli anawapenda Machinga wote nchin, na amekuwa akitutaka viongozi kutowabughudhii na hivyo siye mkoani hapa tunaendelea kuzingatia maelekezo ya Mh Rais kwa utaratibu maalumu"
Aliwataka, wamachinga wote kutumia vema misamaha ya rais yenye nia njema kwa kufuata utaratibu na kukua katika biashara.
“Tuwafundihse Machinga kulipa kodi hata kama ni kidogo, ili kesho wakiwa wafanyabiashara wa Kati au wakubwa wawe tayari wamejenga utamaduni wa kulipa kodi kwa hiari" alisema Rc Chalamila
|