King Majuto anamkubali sana JB

MSANII wa Sanaa za Maigizo na Filamu,  Mzee Majuto ameonesha kuguswa na uigizaji wa msanii wa filamu Jacob Steven, JB.
Mzee Majuto alisema kuwa JB anaweza kutumia vema mwili wake na uwezo wake katika kuwakata kiu washabiki wake.
Alisema kuwa JB anaweza kucheza katika kila kipengele kwenye filamu kuanzia kuwa kama mchekeshaji, mhuni, mnchungaji na mtu wa aina yoyote ile.
Alisema kuwa wasanii kama hao haoa nchini wapo wachache kwa kuwa wasanii wengi wanatabia ya kuchagua kazi za sanaa.
"Huyu jamaa anajua bwana, yani anajua kila anachokifanya kwanza anaigiza kama mwizi, jambazi na sifa nyingine sasa hiki ndo kinachotakiwa kwa kuwa hata katika ile filamu ya Naenda kwa Mwanangu amefanya vema sana humo ndani"alisema Majuto.
Hata hivyo nae JB akizungumzia kazi za mzee Majuto alisema kuwa ni msanii zaidi ya msanii.
Alisema kuwa majuto anajua anachokifanya akiwa katika sanaa na ndio maana anaendelea kuwa msanii wa juu kila kukicha.
"Mimi majuto kwangu ni zaidi ya msanii yani nikiigiza nae kwanza inafika sehemu huwa tunaacha kuimba tunakaa kwanza tunacheka na kisha tunaendelea"alisema JB.

Maoni ya Mhariri

Binafsi nampongeza Mzee Majuto kwa kuwa katika gemu kwa miaka mingi tangia miaka ya 1994 lakini sasa kinachotakiwa kuangalia hapa ni je anajipanga vipi miaka 10 ijayo.

Alikuwa akienda vema hasa katika matangazo ya Luninga akiwa anafanya matangazo ya Airtell na hata ya Azam na alipofariki mwigizaji mwenzake Sharo Milionea ndio na yeye akajikuta akikosa kuendelea tena na matangazo.

Ni vema kwa sasa akatafua Meneja ambae atakuwa akisimamia kazi zake na kumfanya kuwa wa kimafanikio zaidi,

Nakutakia mwaka 2014 mwema na wenye mafanikio

Related

Sanaa 440502178854836203

Post a Comment

emo-but-icon

item