Maridadi Fashion ilivyofunika 2013, ulikuwa mwaka wa shoo nyingi



















Na Mdau wa Mitindo

Mwaka jana ulikuwa ni mwaka wa hafla mbalimbali za mitindo ambapo moja kati ya hafla zilizokuwapo ni pamoja na onesho la Mitindo la Maridadi lililofanyika katika hoteli ya Sleep Way.

 Ni onesho ambalo lilifanikiwa kukusanya milioni tatu kwa ajili ya kusaidia watoto walioathirika na ubakwaji jijini Arusha

.Fedha hizo zilipatikana kutokana na kiingilio kilichokusanywa kwa watazamaji wa onesho hilo lililofanyikia katika hoteli ya Sleep Way, Dar es salaam.
Akizungumza juzi wakati wa onsho hilo mratibu wa onesho hilo Lily Massa alisema kuwa fedha hizo zitapelekwa kusaidia ushauri pamoja na mambo mengine muhimu katika watoto hao walioathiriwa na matukio kama hao mkoani Arusha.
  
Alisema kuwa huu ni mwaka wa nne tangia kuanza kwa onesho hilo ambalo limekuwa kila mwaka lilichangisha fedha hizo za kusaidia watoto hao.

Alisema kuwa kama ilivyokuwa kwa maana ya jina la onesho hilo, Maridadi likiwa na maana kuwa ni mtu imara na ndio wanataka watoto hao kuwa imara katika kupambana na hali hiyo waliyokumbana nayo.

" Yani kwa hawa watoto tunawataka kuwa imara kuwa Maridadi na kuanza tena maisha mapya na ili kufanikisha hilo ni lazima tushirikiane watu mbalimbali kwa njia mbalimbali ambapo njia mojawapo ni hii ya kuchangia kwa njia ya Fashion Show" alisema Lily.

Aliongeza kuwa kwa sasa jamii ya watanzania wanaweza kuchangia fedha kwa kulipia viingilio vya kuona maonesho ya mavazi ambapo wanaweza kujifunza mengi kupitia ujumbe unaowasilishwa katika maonesho hayo.

Naye Mkurugenzi wa Taasisi ya Momella inayojishughulisha na mapambano dhidi ya mauaji ya Tembo, Marlies Gabriel alisema kuwa ametumia onesho hilo la Maridadi kuhamasisha vita dhidi ya mauaji ya Tembo.

" Mimi naona kuwa hii ni fursa yangu kuwavalisha hawa wanamitindo mfano wa meno ya  tembo ikiwa ni inshara ya kupinga mauaji ya tembo na hii napenda wanajamii wote wajue na kupinga pia mauaji ya Tembo" alisema Marlies.

Naye mwanamitindo Suzana Manoko alisema kuwa amevutiwa na shoo ya maridadi kwa kuwa ni tofauti na shoo nyingine kwa kuwa shoo ya Maridadi inalenga kusaidia maisha ya watu wa kila hali.
Mwisho

Related

Burudani 7548034753782178908

Post a Comment

emo-but-icon

item