Video ya Rich Mavoko yaingia kitaa

MSANII wa muziki wa kizazi kipya Rich Mavoko amesema kuwa video yake ya Roho Yangu ilitumia siku nne kutengenezwa.
Mavoko aliiambia safu hii kuwa amekuwa akijipanga kwa muda mrefu kabla ya kuachia video yake hiyo na kuongeza kuwa lengo lilikuwa ni kuhakikisha kuwa anatengeneza kazi nzuri zaidi.
"Najua ni kwamba kwa sasa kuna video nyingi za nyimbo za wasanii na pia kuna hata watengeneza video wengi sasa ilinibidi nijipange kwanza kisha kutoa kazi nzuri kama iliyotokea"alisema Mavoko.
Aliongeza kuwa alilazimika kukodisha Kamera za kisasa kutoka Kenya ikiwa pamoja na kuwakodisha watengeneza video kutoka nchi hizo.
Aliongeza kuwa kwa kuwa wimbo huo unazungumzia maisha ya kawaida ya kila siku hivyo amewahusisha watu wa aina mbalimbali hapa nchini.
Alisema kuwa amewatumia baadhi ya wanamitindo pamoja na wadau wengine katika sanaa kufikisha ujumbe wa wimbo huo ambao kwa sasa ni moja kati ya nyimbo zinazotamba nchini.







Maoni ya MHARIRI


Binafsi naona kuwa msanii huyu anajitaidi lakini kinachotakiwa ni kwa Meneja wake au niseme uongozi wake kujipanga katika kumtangaza na kumweka karibu na watu.

Ni msanii ambae ana nyimbo nzuri yupo katika ngazi kama za akina Ommy Dimpoz na Diamond lakini huyu ajajua namna ya kujiweka kistaa zaidi.

Anatakiwa kuwekewa mikakati ambayo itamnadi zaidi na kumfanya kuwa na swaga za kistaa hapa naweza kumzungumzia msanii kama Barnaba mbali na kuwa na uwezo wa kazi lakini kunakuwa na habari zake za mara kwa mara katka mitandano huku akifanya shoo za mara kwa mara hali ambayo ni nzuri na inazid kumpandisha chati.

Binafsi ningeshauri ajaribu kuiga hata anavyofanya Diamond ana nyimbo nzuri na yeye mwenyewe anaonekana kujitambua kitu ambacho ni muhimu zaidi na kizuri  

Related

Sanaa 7443117122869973234

Post a Comment

emo-but-icon

item