Wanachama Simba waidindia TFF



BAADHI ya Wanachama wa klabu ya Simba wakiongozwa na Albino Rwila,wameyapinga maamuzi ya Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji iliyopo chini ya Shirikisho la soka nchini TFF,kwa kumtambua Ismail Aden Rage kama Mwenyekiti wa klabu hiyo na kumtaka kiongozi huyo aitishe mkutano wa Wanachama wa kujaza nafasi ya Makamu Mwenyekiti iliyokuwa wazi baada ya kujiuzulu Geofrey Kaburu.
Rwila ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa tawi la New Mapambano Temeke Mwisho alisema maamuzi ya Kamati hiyo iliyopo chini ya TFF alisema maamuzi hayo siyo halali ni batili kwa sababu katiba ya Simba inasema endapo kiongozi wa nafasi hiyo atajiuzulu nafasi hiyo inatakiwa kujazwa ndani ya siku 90.
“Kamati ile ilitakiwa kumpa Rage adhabu kwa kushindwa kufuata Katiba ya Simba kwa kushindwa kuitisha uchaguzi mdogo ili kujaza nafasi hiyo kwa sababu hadi jana zimeshapita siku 270 nafasi hiyo haija jazwa hivyo maamuzi hayo kwao siyo sahihi,”alisema Rwila.
Rwila alisema kutokana na madhaifu hayo yaliyoonyeshwa na Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji wao kama Wanachama wa Simba wameadhimia kujihorodhesha ili kudai mkutano wa dharura ambao utakuwa na ajenda mbili ambazo ni uvunjwaji wa Kamtiba ya Simba na pili ni kujadili mstakabali wa marekebisho ya katiba ya Simba kwa mujibu wa maelezo ya TFF.
“Hivi sasa mnavyotuona tupo Wanachama 270 ambao tunataka kudai mkutano wetu kwa mujibu wa Katiba yetu ileile inayosema Wanachama 500,”alisema Rwila ambaye alidai kufuraishwa sana na maamuzi yaliyotolewa awali na Kamati ya Utendaji ya TFF yakumtaka Rage aitishe mkutano nsani ya siku 14.
Rwila alisema Kama Wanachama wenye kuitakia mema klabu ya Simba hawaamuni kinachotekea ndani ya TFF kwani baadhi ya maamuzi mengine yapo kwenye kanuni lakini cha kusikitisha hayafuatwi na Kamatiba ya Simba ni sawa na kwamba imeendelea kukanyagwa.
Wanachama hao walisema endapo maagizo hayo hayototekelezwa wanajua hatua nyingine watakazo fuata ili kuweza kupata haki ya kile ambacho wanakihitaji ili amani ipatikane ndani ya klabu hiyo
Mwisho.

Related

Sport 5451991045394752087

Post a Comment

emo-but-icon

item