Angel aanza mwaka kwa remix

MSANII Angel Karashani ametoa remix ya wimbo wake wa Nisamehe ambapo amemshirikisha msanii Vanessa Mdee.

Pia kwa sasa ameshamaliza kutengeneza Video ya wimbo wake huo ambapo amefanya kazi hiyo na kampuni ya Legendary  Production.

Akizungumza na safu hii Angel alisema kuwa video ya wimb huo inatarajia kutoka wiki mbili zijazo.
Katika kuonesha umakini wa kazi yake alisema kuwa video hiyo imetumia wiki moja hadi kukamilika.

Alisema kuwa ni video ambao nzuri yenye kuendana na ujumbe wa wimbo wake huku akiwa ametumia mazingira yanayoendana na wimbo huo.

Alisema kuwa kwa kuwa wimbo huo ni makini ameamua kuutengenezea marudi mapya (remix) yake kwa kushirikiana na Vanesa ambapo wamefanya kazi kuwa nzuri zaidi.

Related

Sticky 8130734669177846680

Post a Comment

emo-but-icon

item