Bayi alishauri Jeshi


Na Mwandishi wa Blog Hii
KATIBU Mkuu wa Kamati ya Olympic Tanzania (TOC) Philbert Bay amelishauri jeshi kuimarisha mikakati yake ya kusaidia maendeleo ya michezo isiyokua ya soka nchini.

Bay alisema hayo wakati akizungumza na gazeti hili kuhusiana na maandalizi ya Michezo ya Jumuia ya Madola itakayofanyika Julai 23 hadi Agost 3 mwaka huu
.
Bay alisema kwa muda mrefu Jeshi limekuwa mstari wa mbele katika kuninua michezo nchini kutokana na sera zao nzuri za kuinua mivchezo.

Alisema kuwa ili kuwa na timu nzuri za michezo ambayo sio mpira wa miguu basi inatakiwa na mikakati mizuri ya kusaidia maendeo ya wachezaji husika.

Alisema kwa zamani Jeshi lilikuwa na utaratibu wa kwenda kwenye michuano ya shule za Sekondari na kisha wanachagua wanafunzi ambao waneonekana kufanya vema kwenye mchezo husika.

Alisema kuwa kwa kuthamini michezo walikuwa wanawachukua wachezaji hao na kuchukua dhamana nzina ya kuwale iki waje waasaidi tiu zao.

Ali alisema kuwa uamuzi huo ulikuwa ni mzuri kwa kuwa walikuwa wanachukua vipaji na kuniendelezwa.

"Najua huu ni utaratibui mzuri tena sana kwa kuwa kwanza walikuwa wakionekana kuthamini michezo kwa kuwachukuwa wanafunzi na kisha wanawasomesha"alisema Bay.

Akichukulia mfano wa sasa alisema kuwa wapo wanafunzi ambao walichukuliwa katika UMISETA lakini hadi leo hawajasikika kama waliendeel na jesho kama wafanya kazi au la.

Aliongeza kuwa kwa kuwachukua wanafunzi walioonesha uwezo wao katika michezo fulani ni lengo zuri na lenye busara lakini alisisitia kuwa inapaswa wanafunzi hao kuendelezwa zaidi.

Alisema kuwa wapo wanariadha na wachezaji wengine wenye vipaji  waliochukuliwa tangia wakiwa wanasoma elimu ya Sekondari na walifanikiwa kuiwakilisha vema nchi katika michuano ya kimataifa.

Aliongeza kuwa Jeshi lina nafasi nzuri ya kuwaendeleza wanamichezo kutokana na mfumo mzima wa kikazi na inatakiwa kuendeleza jukumu hilo kiufaahsa zaidi.

Alisema kuwa zamani kulikuwa na utaratibu wa Jeshi kwenda katika michuaono mbalimbali ya wanafunzi kama vile Umoja wa Michezo kwa Shule za Sekondari (Umiseta) na walikuwa wakichukua vipaji kadhaa.

Aliongeza kuwa kukosekana kwa hali hiyo kwa sasa inasababisha kushindwa kupatikana kwa vipaji vingi kwa wakati na pia hata wapo ambao walichukuliwa kwa ajili ya michezo lakini walijikuta wakiingizwa kwenye majukumu mengine.

 Akizungumzia maandalizi ya Michezo ya Jumuiya ya Madola kwa sasa alisema kuwa TOC ikiwa kama mshauri na mhusika wa mwisho wa kuchukua timu kwa ajili ya michezo hiyo inaendelea na taratibu za kushauri umuhimu wa kuwa na kambi ndogo na yenye tija.

Alisema kuwa TOC imekuwa ikifanya kazi na wadau wa michezo mingine mbalimbali na hasa imekuwa ikisisitiza suala la umakini katika maandalizi.

"TOC inaamini katika udogo wa watu katika kambi wenye tija kwa kuwa unaweza kuwa na watu wengi lakini ikawa gharama kuwahudumia na kusiwe na tija, hivyo vyama venye kuandaa kambi visijiingize gharama ya kuwa na watu wengi bila ulazima."alisema Bay.

Michezo hiyo kwa mwaka huu itafanyikia katika jiji la Grassrow, Scotland na Tanzania itakuwa moja kati ya nchi 70 zitakazoshiriki michuano hiyo.
Mwisho

Related

Sticky 1737391996301092886

Post a Comment

emo-but-icon

item