Makala: kifo cha MCD na Mzee Dude

HIVI karibuni tasnia ya sanaa ya muziki na maigizo ilikumbwa na pigo kubwa ambalo ni kuondokewa kwa wadau wakubwa katika tasnia hizo.

Alipoteza maisha katika tasnia ya muziki ni mpiga tumba maarufu nchini MCD ambae alifariki katika hospitali ya Kilimanjaro Christian Medical Center (KCMC) iliyopo Moshi.

Kifo hicho kilitokea usiku wa Januari 28 mwaka mwaka huu ambapo alikuwa amelazwa baada ya kusumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu.

Kwa upande wa sanaa ya maigizo aliepoteza maisha ni msanii wa kundi la Futuhi.
Aliepoteza maisha ni mzee Omary Majuto maarufu kama Mzee Dude aliekuwa akisifika zaidi katika kundi hilo la sanaa za maigizo likijihusisha zaidi na masuala ya uchekeshaji.

Wasanii hao wote kwa ujumla walikuwa ni muhimu katika mustakabali mzima wa maendeleo ya sanaa nchini.

Walikuwa na uwezo wa kufanya kazi zao kwa kiwango cha juu huku kila mmoja akiwa na mchango wake katika kampuni au kundi alilokuwa akilifanyia kazi.

Kwa upande wa MCD atakumbukwa zaidi alipokuwa na bendi ya Twanga Pepeta ambapo ilikuwa labda wimbo ukianza au ukiwa katikati ni lazima utasikia jina lake.

Alikuwa ni mmoja kati ya wapiga tumba mahiri nchini ambao wanakumbwa na wataendelea kukumbukwa kutokana na vionjo vyao katika kupiga tumba.

Alikuwa akiipenda kazi yake hasa akiwa katika muziki wa Live jukwaani, alikuwa akitumia filimbi na alikuwa akipiga tumba huku akiruka ruka na kuonesha manjonjo yake yote jukwaani.

Kwa miaka mingi ya nyuma tumba ilikuwa ikichukulika ni kama kifaa cha kawaida kabisa na kisichokuwa na mchango mkubwa katika bendi.

Lakini inaonekana umahiri wa msanii huyu katika kutumia tumba ilifika wakati kabla hata ya wimbo kuanza inasikika tumba kwanza na kisha wimbo unaendelea.

Msanii huyo aliekuwa na bendi ya Twanga awali kabla ya kuhama na kujiunga na dendi ya Mashujaa na kisha kurejea tena Twanga.

Hadi mauti yanamkuta alikuwa katika ziara ya bendi hiyo ya Twanga aliyokuwa akiitumikia bendi hiyo kama Mpiga Tumba.

Kifo cha MCD ni pigo kwa muziki na hasa kutokana na uwezo wake wa kumudu tumba na kuipa hadhi yake inayostahili.  

Simulizi inayouma ya mwanamuziki huyo ilianzia mwishoni mwa mwaka jana ambapo akiwa na bendi yake katika ziara ya kikazi mikoa ya Kanda ya Ziwa.

Hapo ilikuwa wakati bendi yake hiyo ilipokuwa ziarani katika mikoa ya Shinyanga, Mwanza, Kagera na maeneo mwngine katika Kanda ya Ziwa.

Meneja wa bendi ya Twanga Pepeta, Hassan Rehani anasema kuwa baada ya kumalizika kwa ziara hiyo MCD aliomba ruhusua kwa uongozi wa bendi kuruhusiwa kwenda nyumbani kwao Moshi kwa matibabu.

Anasema kuwa uongozi ulimruhusu kurejea nyumbani kwao eneo la Majengo Moshi kwa matibabu na kuahidi kuendelea kuwa nae karibu zaidi.

 “Tulimkubalia kwenda kwao na tulikuwa nyuma yake tukifuatilia hali yake ya maisha ya kila siku"alisema Rehani.

Aliongeza kuwa aliutaarifu uongozi wake kuwa hali yake ya afya ilikuwa ikizidi kuwa mbaya na kuuomba uongozi umsaidie arejee Dar es salaam kwa matibabu na walimtumia nauli ambayo ingemwezesha kufanya hivyo ila alipoteza maisha kablahata ya kuanza safari ya kufika Dar es salaam kwa matibabu.

Meneja huyo alisema kuwa akiwa nyumbani akijiandaa na safari alizidiwa na akakimbizwa hospitalini KCMC alipopoteza maisha.

 “Sasa inaonekana kuwa nauli ile imebidi itumike kumnunulia sanda si ajabu angewahi kusema hali yake si nzuri akatumiwa nauli mapema, akaja Dar mapema leo hii tusingekuwa tunalia".alisema Meneja huyo.

MCD alikuwa ni mmoja kati ya wasanii wachache kutokea mkoani Kilimanjaro na kufanya vema katika sanaa nchini.

Snura Mushi ni msanii mmojawapo ambae ameguswa na kifo cha MCD.

Snura msanii anaetamba na nyimbo zake kama vile Majanga na Nimevurugwa anasema kuwa alikuwa akimsikia MCD tangia miaka ya nyuma akiwa kabla hata hajaanza kuimba.

Anasema kuwa alikuwa akipenda kazi zake na hasa alikuwa ni msanii mwenzake kutokea mkoani Kilimanjaro.

Anaongeza kuwa kifo chake mbali na kuwa pigo kwa uongozi na wapenzi wa Twanga Pepeta na watanzania kwa ujumla kwake anaona kuwa kina mguso wa kipekee kutokana na kuwa alikuwa ni kama msanii ndugu yake kutokana na kutoka mkoa mmoja.

MCD aliezikwa kwenye makaburi ya Njoro, Moshi ameacha mke na watoto wawili.

Kwa upande wa kifo cha Mzee Dude nacho ni pigi hasa kwa wadau wa sanaa za vichekesho.

Ukimzungumzia mzee huyo hasa katika mitaa mbalimbali mkoani Mwanza utasikia sifa zake kuanzia kwa wazee, vijana na watoto kutokana na umahiri wa uigizaji anaouonesha akiwa na kundi la Futuhi.

Kutokana na umahiri wake huo alijizolea umaarufu mkubwa katika kila kona ya nchi.

Mzee huyo alifariki akiwa amelazwa kwenye hospitali ya Bugando alipokuwa amelazwa akipatiwa matibabu kutokana na ugonjwa wa Figo uliokuwa ukimsumbua.

Kwa upande wake msnanii Mzee Majuto anasema kuwa alikuwa akimpenda Mzee Dude kwa kuwa alikuwa akiifanya kazi ya sanaa kwa kuipenda kwa kiasi kikubwa.

Anasema kuwa alikuwa ni mmoja kati ya wasanii wakubwa wa sanaa ambao ni watu wazima na wenye kujua nini wanachokifanya.

"Najua sanaa ya uchekeshaji unakuta ni mara chache sana kukuta wazee wakichekesha na kukubalika katika makundi yote ya vijana na watu wazima na hayo ni mafanikio ambayo Mzee Dude aliyafikia"anasema Majuto.

Vifo vya wasanii hao ni vya kwanza kutokea kwa wasanii wa muziki na maigizo kwa mwaka huu tangia uanze.

Vifo hivi ni vya kwanza kutokea kwa wasanii wakubwa wa sanaa nchini kama hao.

Related

Sticky 5179794661080084144

Post a Comment

emo-but-icon

item