Mchezaji wa Monaco kwenda West Ham, amekaa Monaco muda mfupi kwa usajili wa mabilioni
http://habari5.blogspot.com/2014/01/mchezaji-wa-monaco-kwenda-west-ham.html
MSHAMBULIAJI wa Monaco Lacina Traore aliehamia klabu hiyo akitokea klabu ya Anzhi Makhachkala Jumamosi iliyopita kwa sasa anaonekana kuanza kwa harakati zake za kuhamia klabu ya West Ham.
Mcheza huyo inasemekana kwa sasa anaelekea klabu ya Uingereza na anatafutiwa kibali cha kuanza kucheza soka nchini humo pamoja na kunagaliwa suala zima la afya yake.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi kutoka klabu ya West Ham zinafafanua kuwa mchezaji huyo mwisho mwa wiki ijayo anaweza kuwa ameshakamilishiwa kila kinachostahili ili kuanza kazi nchini humo.
Kwa upande wake klabu ya Monaco ya Ufaransa ilibainisha kuwa ilimsajili Traore kutoka klabu hiyo ya Anzhi Makhachkala ya Urusi kwa kitita cha zaidi ya Bilioni 20 za kitanzania.
Mchezaji huyo alisaini mkataba wa miaka minne na nusu kuitumikia klabu hiyo kubwa ya Ufaransa.
Lakini hata hivyo Monaco imekubaliana na dili hiyo kutoka kwa klabu ya West Ham ya kumchukua mchezaji huyo kwa mkopo.
Kocha wa West Ham, Sam Allardyce ameweka wazi kuwa kikosi chake kinahitaji zaidi kwa sasa msaada wa kuwa na washambuliaji na kuona kuwa kijana huyo anaweza kusaidi.