Moyes" Mata ndio mchezaji wa mwisho usajili msimu huu"
http://habari5.blogspot.com/2014/01/moyes-mata-ndio-mchezaji-wa-mwisho.html
Lakini hata hivyo anakiri kuwa klabu hiyo imekuwa na jitihada za dhati za kusajili wachezaji wengine.
Mata amesajiliwa na klabu yake ya sasa ya Manchester United akitokea klabu ya Chelsea kwa kitita cha zaidi ya bilioni 0 za kitanzania.
Tangia hapo Manchester United imekuwa ikiendelea na harakati zake za kuwanasa wachezaji wengine wakubwa kama vile Luke Shaw wa timu ya Southampton.
Pia wachezaji wengine ambao wamekuwa wakitakiwa na klabu hiyo ni pamoja na Duo Toni na Dante wa Bayer Munich.
Kwa sasa Moyes hana mpango wa kuongeza tena wachezaji na badala yake ataendelea kuwasaidia wachezaji wake ambao ameachiwa na Sir Alex Ferguson.
Moyes alisema kuwa anachitaka kufanya ni kuhakikisha kuwa ana imani kuwa msimu ujao atasajili wachezaji wengi zaidi na wenye viwango.
Mata anaonekana kuwa ni tegemeo kubwa la timu hiyo ambayo imekuwa ikifanya vibaya katika msimu huu wa ligi.
Kwa upande wake akihojiwa na waandishi wa habari wakati akijiunga na klabu hiyo alisema kuwa anatarajia kuonesha soka safi ambalo wapenzi wa klabu hiyo wamekuwa na shauku ya kuliona kwa muda mrefu.