Baba mzazi wa Messi akanusha mwanawe kuihama Barcelona
http://habari5.blogspot.com/2014/01/baba-mzazi-wa-messi-akanusha-mwanawe.html
WAKALA wa mchezaji Leonel Messi, Jorge Messi ambae ni baba yake mzazi amesisitiza kuwa mchezaji huyo hatoihama klabu ya Barcelona na kujiunga na klabu ya Paris Saint - German au klabu yoyote ya Ujerumani kwa miaka ya hivbi karibuni.
Klabu hiyo ya Paris inasemekana kuwa imeandaa kitita zaidi ya bilioni 500 kwa ajili yaskufanikisha usajili wa Messi katika msimu huu.
Wakala huyo alikaa kusikiliza ofa hiyo kutoka klabu hiyo iliyokuwa ikimtaka mwanawe huyo kujiunga nao na alisisitiza kuwa mwanawe kamwe hatohama klabu hiyo hivi karibuni.
Wakala huyo aliliambia jariba la L'Equipew kuwa amekuwa akisikia fununu pia kutoka kwa watu mbalimbali wakielezea madai hayo ya kuwa mchezaji huyo ataihama klabu yake ya Barcelona.
Alisema kuwa kwa sasa mchezaji huyo ana mkataba na klabu ya Barcelona hado kufikia mwaka 2018.
"Kwa sasa hilo sio suala la sisi kulifikiria, hatuna haja ya kujadili kuhama kwa mchezaji huyu kwenda PSG lakini pia ninaiheshimu sana klabu hii ya PSG"alisema Jorge Messi.
Alisema kuwa mkataba wa mchezaji huyo na klabu ya Barcelona hadi mwaka 2018 ni mkataba muhimu kwake na kwa sasa sio wa kwenda PSG au kokote kule.
Lakini hata hivyo baba yake huyo alikiri kua hana uhakika kuwa mchezjai huyo ataendelea kuitumikia Barcelona hata baada ya kumalizika kwa mkataba wake.
"Najua kuwa kwenye mpira hakuna mtu wa kuweza kujihakikikishia kuhusiana na kesho sasa kinachotakiwa kuzingatiwa hapa ni kwamba inaweza akalazimika kuhama iwapo muda ukifika"alisema Jorge Messi.
Messi alijiunga na klabu ya Barcelona akiwa na miaka 13 ambapo alianza kuchezea katika timu ya watoto.
Tangia ajiunge na timu ya wakubwa ameipatia mafanikio makubwa timu hiyo kwa kuifungia magoli 313 katika michezo 400.