Ay kupiga kazi na Jagwa

MSANII Ambwene Yesaya, AY pamoja na Ommy Dimpoz wamerekodi wimbo na msanii Jagwa wa Kenya.

Ay akizungumza na safu hii alisema kuwa Jagwa alikuwa hapa nchini kwa siku tatu akirekodi moja kati ya nyimbo zake.

Alisema kuwa kwa sasa hawezi kuwek awazi jina la wimbo huo kwa kuwa kuna vitu vinaendelea kufanyika.

"Najua Jagwa ni msanii mkubwa sana kule Kenya na kwa sasa anatamba na wimbo wake uitwao Kioo, ambao video yake ilikuwa gumzo kubwa hapa nchini pia sasa kuna kazi ambayo inakuja na itakuwa nzuri zaidi"alisema AY.

Aliongeza kuwa kwa sasa wasanii wengi wa Kenya wanazidi kuja juu na kufanya muziki wenye faida zaidi.

Alisema kuwa katika kuleta mafanikio ya kweli kwenye medani ya muziki Afrika Mashariki inatakiwa wasani wa hapa nyumbani kuwashirikisha wasanii kama wa Kenya, Uganda na hata Rwanda.

Related

Sticky 1716830323756911839

Post a Comment

emo-but-icon

item