Barnaba afagilia makampuni ya Ringtone

MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Elias Barnaba ameonesha kufagilia hatua ya makampuni mengi kujitokeza na kununua nyimbo za wasanii na kuziweka kama milio ya simu.

Barnaba alisema kuwa kuongezeka kwa makampuni hayo inaongeza ushindani na hatimae kuwanufaisha wasanii wa nyimbo husika.


Alisema kuwa awali kulikuwa na makampuni machache yaliyokuwa yakijishughulisha na uuzaji na ununuzi wa nyimbo hizo hali iliyokuwa ikiwafanya wasanii kunyenyekea kwenye kampuni hizo chache.


Aliongeza kuwa kwa kuongezeka kwa makampuni hayo kwa sasa inasaidia wasanii kupata fedha nyingi zaidi kwa kuwa iwapo kampuni moja ikishindwa kulipa vizuri na kwa wakati msanii anaweza kwenda kampuni nyingine.


"Najua unaweza kujikuta msanii unapiga hela nyingi zaidi kupitia nyimbo zetu kutumiwa kama ring tone na kujikuta kama msanii unakuwa na kipato kizuri zaidi hasa pale ambapo unakuwa na wimbo mzuri na ukanunuliwa sana"alisema Barnaba.


Aliongeza kuwa kwa upande wake amekuwa akinufaika kupitia Ringtone hizo na kuongeza kuwa hata kama msanii akikaa mudamrefu bila shoo lakini anaweza kupata fedha kupitia milio hiyo.

Related

Sticky 7207438099942621133

Post a Comment

emo-but-icon

item