Tigo yachukua tahadhari na jengo lake


Tigo Tanzania leo imeonyesha ni jinsi gani inajali wafanyakazi wake kwa kuchukua tahadhari na kufunga ofisi zake za makao makuu yaliyopo kwenye jengo la Derm House lililopo barabara ya Ali Hassan Mwinyi kufuatia kugundulika kuwa vigae vichache vya sakafu ya ghorofa ya nne ya jengo hilo vimevunjika.

Kutokana na habari iliyotolewa na mkuu wa operesheni za Tigo Bwana Deon Geyser Tigo
wafanyakazi wote wa ofisi za Tigo na wale wa duka la huduma kwa wateja lililopo jengoni hapo waliagizwa kuondoka kwenye jengo ili kuruhusu uchunguzi zaidi utathmini sababu ya uvunjikaji huo wa vigae.

“Tuliagiza wafanyakazi wetu wote waondoke kweye jengo kufuatia kanuni zetu za utendaji za usalama wa wafanyakazi ambazo zinathamini usalama wa wafanyakazi kama jambo muhimu zaidi kwenye biashara yetu. Hatuchukui jambo lolote linalohusika na usalama wa watu wetu juu juu hata kama linaonekana ni dogo na halina uzito sana.” Bwana Geyser alisema kwenye maelezo yaliyotolewa kwa wanahabari na kapuni hiyo. Aliongeza kuwa hakuna madhara yeyote yaliyotokea kwa wafanyakazi wala kwa vifaa au jengo hilo.

“Tunataka kuwahakikishia wateja wetu wote na wananchi kwa ujumla kuwa ukiachana na kufungwa kwa muda kwa ofisi za makao makuu, maduka yetu yote mengine ya huduma kwa wateja jijini Dar es Salaam na nchi nzima yanaendelea kufanya kazi na kutoa huduma bora kabisa kwa wateja wetu wapendwa.” Aliendelea kusema.


Maelezo ya Bwana Geyser yameeleza kuwa Tigo ilihamishia ofisi zake za makao makuu kwenye jengo la Derm House mwaka 2012 na kwa muda wote huu hakujawahi kutokea tukio lolote linalohusiana na usalama wa jengo hilo la aina yeyote ile. Ghorofa zote nane za jengo la Derm  House zimekodishwa na ofisi ya Tigo pekee.

“Baada ya uchunguzi kufanyika, ripoti zote za wahandisi zinasema kuwa jengo liko salama kwa matumizi, na hivyo shughuli zote zitaendelea kama kawaida. Wafanyakazi wote watarudi ofisini na duka la huduma kwa wateja kufunguliwa kesho”, alikamilisha Bwana Geyser.

Related

Sticky 2234885875568330230

Post a Comment

emo-but-icon

item