Mwaka huu yawepo mabadiliko ya kweli kwenye michezo
http://habari5.blogspot.com/2014/01/mwaka-huu-yawepo-mabadiliko-ya-kweli.html
NI siku chache tu zimepita tangai kuingia kwa mwaka mpya wa 2014 ambapo binafsi napenda kuzungumzia masuala ya maendeleo ya michezo kwa mwaka huu.
Kama ilivyo kawaida kwa kila mwaka kunakuwa na mikakati mipya katika kuimarisha mambo mengi muhimu katika sekta mbalimbali.
Sekta kama vile za uchumi, uchukuzi, na nyinginezo muhimu zinaweka wazi vipaumbele vyake kwa mwaka huu.
Binafsi napenda kuchukua fursa hii kuwataka wadau wa michezo mbalimbali nao kuwa na mikakati mipya ya kuimarisha maendeleo ya michezo yao.
Hapa nikiwa na maanisha kuwa wawe na mikakati ambayo itasaidia kuleta mabadiliko katika medani ya michezo hapa nchini.
Katika kulifanikisha hili ni sio tu kwa kuwa na mikakati mipya peke yake bali hata kuwa na mbinu mpya za kuendeleza mikakati ya zamani.
Mikakati ikiimarishwa vema ndio inayoweza kuleta mapinduzi katika michezo ya aina yoyote ile.
Mfano mzuri ni mkakati ambao klabu ya Yanga imekuja nao ambapo ni kuweka viongozi wapya wa benchi la ufundi ambapo kuwatoa akina kocha mkuu Enerst Brandits na Fred Minziro na wengine na kisha kuwaweka akina Charles Mkwasa kama kocha msaidizi na kocha wa makipa Juma Pondamali.
Harakati kama hizo ni ambayo inakuwa na nia ya kuleta mabadiliko ambapo naona kuwa ni mikakati ambayo inatakiwa kuimarishwa na hata klabu na vyama vya soka.
Sina maana ya kuwa nao wafanye mabadiliko kama lakinibasi angalau kwa kuwa na nia ya kweli ya kufanya mabadiliko yenye kuleta tija.
Mfano katika vyama vya michezo utakuta kuna madudu ambayo yalikwamisha maendeleo ya vyama hivyo lakini hakuna nia ya kufanya mabadiliko ya kweli ya kuondokana na tatizo husika.
Pia sio tu mabadiliko ya utendaji ndio peke yake yanaweza kuleta mabadiliko lakini pia hata katika kubadilika kwa wachezjai wenyewe.
Suala la uwajibikaji na nidhamu ni suala la msingi kwa kuendeleza kila mchezo hapa nchini.
Wapo wachezaji wa michezo mbalimbali ambao hawazingatii nidhamu kama njia mojawapo ya kuendeleza michezo husika.
Nidhamu ya kujituma katika kazi inakosekana na hivyo kurudisha nyuma adham nzima ya kusonga mbele kwenye kuendelea michezo.
Wapo wachezaji ambao kwanza wanaona kuwa ni kitu cha kawaida kwao kuchukua ruhusa ya kuumwa ili kukwepa mazoezi
Hii inapelekea kushuka kwa maendeleo ya mchezo kwa kuwa wachezaji wanatumia muda mwingi kuendekeza ugonjwa ambao haupo badala ya kufanya kazi.
Wapo ambao pia wanashirikiana na hata viongozi wa timu au vyama husika kukwepa kufanya mazoezi.
Ili kukabiliana na hali hiyo inatakiwa kwanza kwa viongozi wenyewe wa michezo husika kubadilika kiutendaji kwa mwaka huu wa 2014.
Wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanapambana na kila aina ya ubabaishaji michezoni.
Jana Kocha Pondamali aliwasema hadharani makipa timu ya Yanga kwa kuukosoa uwanja wa Bora kuwa hauna mazingira mazuri ya kufanyia mazoezi ambapo alisisitiza kuwa haitaji mzaha wa aina hiyo katika kufanya kazi yake.
Mifano ya makocha kama hawa ndio mizuri katika kuimarisha michezo mwaka huu kwa kuwa kwanza anawatoa wachezaji hao katika kujiona kuwa ni kila kitu na kudharau kazi.
Umakini wa makocha kama huu ndio unatakiwa kwa mwaka 2014 kwa kuwa ndio unaweza kuongeza umakini kwa wachezaji hasa wakiwa mazoezini na michezoni.
Kwa pamoja tunaweza kuiwezesha sekta ya michezo nchini kufika mbali zaidi hasa kwa kuanza na mwaka huu wa 2014.
Mwisho