Nani Mbabe kati ya Arsenal na Fullham jumamosi hii

TIMU za Fulham na Arsenal zinacheza leo katika Ligi Kuu England huku mara kwanza kukutana ikiwa ni mwaka 1904 hivyo kuwa na takribani miaka 110 hadi sasa.

Timu hizo zilikutana kwenye Ligi Kuu hiyo ya England mwaka 1904 Arsenal ilishinda kwa 3-2.
Baada ya kukutana tena kwa takriban mara 26 katika uwanja wa Arsenal, Fullham haikuwahi kushinda na kujikuta ikiambulia kipigo kutoka kwa Arsenal.

Hivyo kufuatia historia hiyo leo hi Fullham inakumbana tena na Arsenal ambayo imecheza ligi hiyo bila kufungwa katika kiwanja cha nyumbani tangia kuanza kwa ligi.

Arsenal hiyohiyo ndio hadi sasa inaongoza katika ligi kuu huku ikiwa imejiimarisha kileleni.

Kikubwa ambacho kinaonekana kuipatia Arsenal mafanikio hayo ni ushirikiano imara katika suala zima la ulinzi ambalo limeiwezesha kushinda magoli sita katiak mechi 10 za ligi kuu katika uwanja wao wa Emirates Stadium.

Fulham iliwahi kuchezea kichapo kutoka kwa Hull City lakini hata hivyo ushindi wao dhidi ya timu ya West Ham na ule dhidi ya Norwich City katika ligi kuu England imewaongezea hali ya ushindi wachezaji wa timui hiyo.

Kwa sasa kikosi hicho kinaonekana kujiamini zaidi baada ya kurejea kwa beki wake Brede Hangeland.

Ujio wa mchezaji huyo ulisaidia timu hiyo ya Fullham kuibuka na ushindi wa 3-0 katika mchezo wa Jumatano iliyopita dhidi ya timu ya Norwich kwenye Ligi Kuu England

Mchezaji huyo ambae alikuwa nje ya uwanja tangia mwezi Oktoba mwaka jana kufuatia jeraha la mguu alilopata na tangia arejee amekuwa msaada mkubwa kwa timu hiyo.

Ameisaidia Fulham kufanya vema katika mechi zaidi ya nane tangia arejee na kwa sasa anaonekana kuwa ni msaada mkubwa kwa timu hiyo katika mchezo wake wa leo dhidi ya Arsenal.

Kwa Arsenal itacheza huku ikiwa haina mchezaji wake Theo Walcott ambae aliumia hivi karibuni na hivyo kukosa mechi kadhaa zijazo za Ligi Kuu ikiwa hiyo dhidi ya Fullham.

Wengine ni Mikel Arteta, Nicklas Bendtner, Aaron Ramsey na Thomas Vermaelen.
============================

Related

Sticky 8249104941564197334

Post a Comment

emo-but-icon

item