Madonna akanusha kuwa mbaguzi

MWANAMUZIKI Madonna amekanusha tetesi kuwa ana tabia ya kibaguzi.

Hiyo imekuja kufuatia kulalamikiwa na watu katika mtandao wa kijamii wa Instagram kufuatia ujumbe alioandika kwenye picha ya mtoto wake.


Katika picha hiyo ya mtoto wake wa miaka 13 wa kiume, Rocco Ritchie Madonna aliandika ujumbe wenye inshara ya kuonya mtu yoyote atakayecheza na sabuni chafu atakiona cha moto.
 

Aliandika ujumbe akifafanua kuwa alikuwa hana nia ya kukashfu wala kukejeli lolote katika ujumbe wake huo.
Aliongeza kuwa kwa upande wake sio mbaguzi wa rangi na wala hana tabia za kibaguzi na hivyo kuwataka washabiki wake kutomwelewa vibaya.


Hata hivyo alifikia uamuzi wa kuifuta picha yake hiyo katika Instagram ili kuondoa mtafaruku huo na kusisitiza kuwa hakua na nia mbaya katika hilo.


Alisema kuwa kwa kuandika ujumbe wa kusema mtu asicheze na sabuni chafu hakuwa na maana kuwa mwanawe ni  mchafu au kuwa na maana ya kuwa mtoto wake asiwe karibu na watu.


Related

Sticky 4222268890225686381

Post a Comment

emo-but-icon

item