J Lo anampango wa kuolewa na dansa wake
http://habari5.blogspot.com/2014/01/j-lo-anampango-wa-kuolewa-na-dansa-wake.html
MWANAMUZIKI Jennifer Lopez wa Maarekani huenda mwaka huu akafunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu Casper Smart.
Kwa kawaida katika historia ya Hollywood wapenzi kama hao ambao wanakaa zaidi ya muda wa miaka mitatu kwao wakiwa wapenzi ni inshara tosha ya ndoa kwa wapenzi husika.
Kwa Jennifer ambae ameolewa mara tatu na kuchumbiwa mara moja inaonekana kuwa uhusiano wake wa sasa itakuwa ni ndoa yake nyingine.
Katika mahojiano yake na Jarida la E, Lopez alisema kuwa yeye ni mmoja kati ya watu wanaoamini kwenye uhusiano wa muda mrefu akiwa anaaminisha kuwa ndoa.
Akizungumzia uhusiano wake na kijana huyo alisema kuwa anaona kuwa ni muda wao kuwa na maisha yao ya pamoja.
Lakini hata hivyo mbali na kushindwa kuweka wazi ni lini hasa anaweza kutangaza kufunga ndoa na kijana huyo dalili zinaonekana kuwa huenda wakafanya hivyo muda mfupi ujao.
Kwa mujibu wa jarida la E, Jennifer amekuwa akionekana mara kwa mara akiwa na kijana huyo hasa katika mitoko mbalimbali nchini Marekani.
Na pia pete ya uchumba ambayo amevalishwa na kijana huyo ni inshara ya kuwa mambo yatakuwa hadharani muda mfupi ujao.