Wojciech Szczesny alimpigania Robert

KIPA wa timu ya Arsenal,  Wojciech Szczesny amesema kuwa alijiataidi kwa kiasi kikubwa kumshawishi mchezaji Robert Lewandowski kujiunga na timu yake hiyo.

Mchezaji huyo alikuwa akitakiwa na Arsenal lakini hata hivyo alitoka klabu yake aliyokuwa akiichezea ya Borussia Dortmund kwenda  Bayern Munich.

Mchezaji huyo ametumia msimu huu wa usajili kuhama kutoka klabu yake hiyo na kuichezea Bayern Munich.
   
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger kwa upande wake alithibitisha kumhitaji kwa kiasi kikubwa mchezaji lakini juhudi zake hizo kushindwa kuzaa matunda.

Pia kwa upake wake kipa Szczesny alisema kuwa Lewandowski ni rafiki yake wa muda mrefu na alikuwa akihitaji kucheza naye kwenye timu ya Arsenal.

"Ni rafiki yangu mkubwa ambae tunacheza nae katika timu ya taifa, ni rafiki yangu wa muda mrefu tu, na nimefanya kila niwezavyo kumshawishi kujiunga na timu yetu hii"alisema kipa huyo.

Related

Michezo 2926705181394757778

Post a Comment

emo-but-icon

item