Viongozi wa michezo wamfagilia Nkhamia

Na Mwandishi wa Habari Leo  
MWENYEKITI wa Klabu ya Simba, Ismail Rage amempongeza Naibu Waziri Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Juma Nkamia kwa kuchanguliwa kushika nafasi hiyo.


Nkamia ni Mbunge wa Kondoa Kusini na aliwahi kuwa Katibu Mwenezi wa klabu ya Simba miaka ya nyuma kabla ya kuwa Mbunge.


Lakini hata baada ya kuwa mbunge bado aliendelea na harakati za kusaidia klabu hiyo ambapo aliwahi kuchaguliwa kuwa mjumbe wa kamati ya Fedha ya Simba.


Akizungumza na gazeti hili Rage alisema kuwa kwa upande wake anampongeza Nkamia kwa kuwa ni mwanamichezo hai na mwenye shauku ya kuona soka ikisonga mbele.


Alisema kuwa Nkamia amekuwa akitoa ushauri mara kwa mara katika masuala ya soka na ana imani kuwa atasaidia kwa kiasi kikubwa sekta ya soka na michezo kwa ujumla.


"Mimi ninampongeza Rais Kikwete kwa kumchangua Nkamia kwa kuwa ameipatia sekta hii mtu muhimu na makini kwa kiasi kikubwa na kwa niana ya Simba ninamtakia mafanikio mema"alisema Rage.

"Kwa hata pale Bungeni mara nyingi akisikia kuwa mambo yamekuwa mabaya klabuni Simba Nkamia amekuwa hasiti kunielekeza mengi ya kufanya ili kutatua changamoto za hapa na pale na nina imani kuwa hata katika michezo mingine atafanya hivyo  kwa kuwa huyu ni mwanamichezo"alisema Rage.

Pia Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Tennis Tanzania, Fina Mango alisema kuwa ana imani kuwa Naibu Waziri huyo ataitazama michezo mingine ambayo sio soka.


Alisema kuwa Tennis ukiwa kama mchezo kati ya michezo inayokabiliwa na changamoto nyingi inahitaji kusaidiwa kwa hali na mali na anaona kuwa Nkamia kama Naibu Waziri ambae ni mdau wa michezo atafanya hivyo.


"Mimi naona kuwa huyu Naibu atakuwa msaada mkubwa pia katika kusukuma mafanikio ya michezo kama hii ambayo sio mpira wa miguu, nachukulia mfano katika mchezo wa Tennis huyu atakuwa ni msaada mkubwa kwetu katika Tennis"alisema Fina.


Kwa upande wake Katibu wa Shirikisho la Ngumi Tanzania, Makore Mashaga alisema kuwa anaona Rais Kikwete amefanya uamuzi mzuri wa kumchangua mtu ambae amekuwa akijihusisha na michezo kwa muda mrefu.


Alisema kuwa akiwa kama mwanamichezo atakuwa karibu zaidi na wadau wa michezo mingine mingi na kusaidia kufanikisha maendeleo ya michezo kwa ujumla.


"Huyu ikikumbukwe kuwa alikuwa na pia ni bado anajihusisha na michezo kwa namna mbalimbali akiwa kama mwanasiasa, sifa zake alizonazo katika michezo zinamfaa kabisa kuwa Naibu katika Wizara hii yenye dhamana ya Michezo"alisema Mashaga.

Nkhamia anachukua nafasi ya Amos Makalla aliekuwa Naibu Waziri Wizara hiyo.


 Nkhamia ambae kitaaluma ni mwandishi wa habari amewahi kufanya kazi na Mashirika ya Habari ya Utangazaji makubwa duniani kama vile Voice of America, BBC na pia amewahi kufanya kazi kama mhariri wa habari za biashara wa Shirika la Utangazaji la Taifa, TBC.
Mwisho


Related

Sticky 1405216138536512584

Post a Comment

emo-but-icon

item