Oprah asherehekea birthday yake kimaskini

MTANGAJI Mahiri w avipindi vya Luninga wa nchini Marekani Oprah Winfrey amefanya sherehe ndogo ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa iliyofanyika juzi.

Oprah alifanya hafla hiyo katika kusherehekea miaka 60 ya kuzaliwa katika nyumba yake iliyopo northwest of Los Angeles.


Tofauti na ilivyokuwa ikifikiriwa mara nyingi kuwa huenda sherehe hiyo ingekuwa kubwa zaidi kutokana na Oprah kusikiwa mara kwa mara akisisitiza nia yake ya kuifanya sherehe yake hiyo kuwa kubwa.


Mwanamama huyo ambae ni mmoja kati ya wanawake wenye ushawishi mkubwa kwa sasa duniani akiwa na utajiri wa zaidi ya trilioni 2 amekuwa mara kwa mara akizungumzia kuwahamasisha wanawake kufanikiwa kwa kutumia namba 6.


"Mara kwa mara huwa ninaitumia namba ya 6-0 ni kama namba ya ushindi kwangu na nimekuwa nikiwasihi watu kuichukulia namba hiyo hivyohivyo"alinukuliwa Oprah.


Kutokana na hiyo watu wengi walikuwa wakiichukulia ni sherehe yake ya miaka 60 kuwa ingekuwa kubwa na yenye kuendana na kampeni ya kusaidia watu wengi zaidi.

Related

Sticky 6025741918714013159

Post a Comment

emo-but-icon

item