Omotola akerwa na machafuko Nigeria

MWIGIZAJI  mahiri wa kike wa Nigeria Omotola Jalade-Ekeinde ameonesha kukerwa na hali mbaya ya usalama kwenye eneo la Niger Delta.

Msanii huyo ambae akuwa akijihusisha na uigizaji wa filamu pamoja na uimbaji wa muziki amekuwa akijikita zaidi katika kusaidia masuala mbalimbali ya kijamii nchini humo.


Pia ni balozi wa Umoja wa Mataifa katika kupigania amani sehemu mbalimbali duniani.


Akiwa kama mwakilishi wa shirika hilo Omotola alisema kuwa kwake anaona kuwa hakuna sababu ya kuendelea kwa mchafuko hayo katika eneo hilo.me


Alisema kuwa ana nia ya dhati ya kuhakikisha kuwa anarejesha hali ya amani katika eneo hilo linalokabiriwa na uvunjifu wa amani.


Eneo hilo limekuwa na machafuko mara kwa mara kutokana na kuwa na utajili mkubwa wa mafuta huku wananchi wake wakihangaika kwa kukosa mahitaji muhimu.


Hali hiyi imepelekea vita vya muda mrefu huku wnanachi wa eneo hilo wkaitaka kujitenga lakini kwa sasa serikal imekuwa ikijitaidia kuzuia hali hiyo.


Kutokana na hali hiyo uamuzi wa Omotola kupigania hali ya amani katika eneo hilo inaweza kusaidia harakati za serikali pia katika kupambana na hali hiyo.
====================================



Related

Sticky 3869462863676342564

Post a Comment

emo-but-icon

item