Ponda Malii "mikwara kibao"


KOCHA Mpya wa Makipa wa Yanga Juma Pondamali jana alionekana kuanza kwa mikwara kuwanoa makipa wa timu hiyo iliyokuwa ikifanya mazoezi kwenye uwanja wa Bora Kijitonyama.
Pondamali katika kuonesha umakini katika ufundishaji wake, aliiwaambia waandishi wa habari kuwa hatoruhusu makipa kumwaribia kibarua chake.

Alisema kuwa makocha walioondoka hawakuwa wabaya ila inaonekana kuwa kulikuwa kuna mzaha ambao hakufanyiwa kazi na ndio maana ikaja kuwagharimu.

Pondamali alisema hayo alipokuwa akijibu maswali ya waandishi wa habari kuhusiana na namna alivyowatathmini makipa hao.

Alisema kuwa walikuwa wakiulalamikia uwanja kuwa ni mbaya na sio mzuri kwa mazoezi.
Alisema kuwa kwake hivyo ni visingizio visivyokuwa na umuhimu kwa kuwa kinachotakiwa ni mazoezi yenye tija.

"Najua sio kwamba walioondoka hawakuwa na uwezo hapana ila mizaha kama hii ndio inaonekana kuwa kikwazo sasa mimi hiyo sina kabisa yani nimekuja hapa kupiga mzigo na sio masuala ya kuremba"alisema Pondamali.

Alisema kuwa hata hivyo alikuwa amepanga kuwafundisha aina 12 za mazoezi lakini alilazimika kuwafundisha aina nane na nyingine atazimalizia leo asubuhi.

Lakini hata hivyo alisema kuwa anajisikia furaha kuwanoa makipa hao hao kwa kuwa mara kwa mara anakuwa nao katika timu ya taifa.

Pondamali  amechukua nafasi ya Razak Siwa ambae nae alipewa mkono wa kwaheri, jana katika mazoezi hayo aliwafundisha makipa Juma Kaseja,Deogratias Munish na Ali Mustapha.
Mwisho
  

Related

Sport 7100634793836354666

Post a Comment

emo-but-icon

item