Tukio la sanaa lililonigusa 2013
http://habari5.blogspot.com/2014/01/tukio-la-sanaa-lililonigusa-2013.html
Na Mwandisho Wetu
Mwaka 2013 wasanii wa sanaa za uchoaji 10 waliungana kwa pamoja na kumuunga mkono Mustahiki Meya wa Ilala Jery Silaa katika kusaidia upatikanaji wa madawati ya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari.
Akizungumzia uamuzi huo mratibu wa wasanii hao Robert Ntilo alisema kuwa kama wasanii wameguswa na harakati za Meya na kuamua kusaidia kwa njia ya kuuza kazi zao za sanaa.
Alisema kuwa kupitia kazi za sanaa wanaweza kuuza picha zao ambapo fedha zinazopatikana kwa njia hiyo ya mnada zikatumika kusaidia upatikanaji wa madawati.
" Najua sanaa ina nguvu na hasa hii sanaa ya michoro ina nguvu ambayo inaweza kwa kiasi kikubwa kusaidia kuleta mabadiliko, sasa kwa kujua kuwa picha zinaweza kusaidia kutatua matatizo ya madawati basi tunaona kuwa hii ndio njia yetu kubwa katika kusaidia" alisema Ntilo.
Kwa upande wake Meya Silaa alisema kuwa wasani hao watakuwa katika kambi ya siku tano wakichora michoro mbalimbali ambayo itakuja kuuzwa kwenye hafla ya chakula cha mchana itakayofanyika Novemba 16 mwaka huu.
Alisema kuwa zinahitajika shilingi za kitanzania bilioni 4.98 kwa ajili ya kununulia madawati kwa ajili ya shule za msingi na sekondari 30,487 za Manispaa hiyo.
Alisema kuwa wasanii wa sanaa za uchoraji wamefungua njia kwa watu wengine kujitokeza kuangalia namna ya kusaidia.
" Najua mwisho wa siku hawa sio watoto wa Jerry Silaa au wala sio jukumu la Mheshimiwa Raisi peke yake ila ni suala letu wote hivyo kama wasanii hawa wameamua ni kwa nini ishindikane kwa wengine" alihoji Silaa.
Wasanii wanaoingia katika kambi hiyo ni pamoja na Robino Ntila, Aggrey Mwasha,SalumKambi,Cuthbert Mgonja, James Haule na Haji Chilonga.
Wengine ni Thobias Minzi,MosesLuhanga,Pomi Yengi Miss,Vita Malulu na James Haule.
Maoni ya Mhariri
Binafsi naona kuwa Meya Jerry muda mwengine anakurupuka na kuanzisha vitu vingi sana ambavyo huenda mwisho wake ukawa sio mzuri.
Sasa harakati hizo mbona naona kuwa kwa saa ni kama kimya na hakuna mwendelezo wowote, jipange Kaka kwa kuhakikisha kuwa unakuwa na mikakati ya kufanikisha kutumiza ndoto zako