Rushwa na Ubabaishaji vinaathiri kukua kwa michezo nchini
http://habari5.blogspot.com/2014/01/rushwa-na-ubabaishaji-vinaathiri-kukua.html
Rushwa, Ubabaishaji na Ushirikina vinavyorudisha nyuma maendeleo ya soka.
Na Mwandishi wa Michezo
KWA muda mrefu hapa nchini kumekuwa na harakati mbalimbali za kusaidia kuinua michezo ya aina mbalimbali kama vile soka, netiboli, kikapu na mingineo.
Harakati hizi zimeongezwa chachu na makampuni mbalimbali yakiwamo makampuni ya vinywaji na makampuni ya simu.
Harakati hizi zimesaidia kwa kiasi kikubwa kuleta mabadiliko katika sekta ya michezo hasa kwa kuongeza hamasa ya wananchi kujiingiza kwenye fani hiyo.
Lakini harakati kama hizo kutoka kwa wadau wa michezo, wadhamini, serikali na hata watu binafsi zinaonekana kukutana na vikwazo mbalimbali kama vile Rushwa, Ubabaishaji na imani za kishirikisha.
Rushwa imejijengea mzizi mikubwa katika michezo na kupunguza nguvu za harakati za maendeleo ya sekta hiyo. Mbali na uzito wa tatizo hilo lakini bado inaonekana kuwa rushwa katika michezo haitazamwi kama tatizo kubwa.
Kumekuwapo kwa tuhuma mbalimbali zikiwakabili wachezaji kuhusika na kuuza mechi au kucheza chini ya kiwango kwa malipo ambayo wamekuwa wakipewa na timu pinzani.
Lakini katika kukabiliana na hilo mpaka sasa hakuan mifano hai ya wachezaji ambao wametiwa hatiani iwe katika vyama vya michezo husika au hata katika mahakama za kiraia.
Pia wapo wachezaji ambao waliwahi kukiri hadharani kuhongwa fedha ili wacheze chini ya kiwango kwa kuiwezesha timu pinzani kushinda.
Mchezaji wa soka Nsa Job ni mmoja kati ya wachezaji waliowahi kukiri hadharani kuhongwa fedha ili wacheze nje ya kiwango lakini hadi sasa hakuna taarifa kuhusiana na hatua za kisheria kuchukuliwa na dhidi yake.
Katika kukabiliana na aina kama hii ya rushwa na nyinginezo, Katibu wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo nchini (TASWA) Amir Mhando anasema kuwa waandishi wa habari wana nafasi kubwa ya kupambana na rushwa michezoni.
Anasema kuwa waandishi wa habari hawapaswi kuwa watu wa kupokea habari, kuziandika na kuziacha tu lakini badala yake wanatakiwa kuingia kiundani kwa kuzifuatilia ili kujua hatma yake.
Anatolea mfano wa tuhuma mbalimbali za rushwa zinazowakabili waamuzi wa soka, anasema kuwa kuna wakati kwa mwandishi wa habari hata akiwa anautazama mchezo anaweza kujua kabisa kuwa uchezeshaji wa mwamuzi huyu una ualakini na inatakiwa kuchunguza ili kujua mazingira ya rushwa kwa mwamuzi husika.
"Maendeleo ya michezo yoyote ile yanachangiwa na nguvu kutoka kwa waandishi wa habari sasa iwapo sisi tukishindwa kutimiza wajibu wetu katika kupambana na rushwa na ubabaishaji michezoni basi hakuta kuwa na mafanikio ya kweli katika kukuza michezo nchini"anasema Mhando.
Anasema kuwa rushwa michezo imekuwa ni kama kitu cha kawaida tu hasa pale ambapo wakati wa chaguzi mbalimbali za vyama vya michezo utakuta watu wakiongana na waandishi wanashindwa kutazama hilo ni kama mojawapo ya vitu ambavyo vinaweza kuwa chanzo cha kushuka kwa michezo.
Kuwepo kwa viongozi wa vyama vya michezo wanaoingia madarakani kwa rushwa ni chanzo kingine kinakwamisha maendeleo ya michezo.
Hapo ndipo linapozuka suala la ubabaishaji ambalo ni chanzo kingine cha maendeleo ya michezo nchini.
Hawa wakishaingi madarakani ndio wanakuwa wanatumia muda wao mwingi kufanya majungu na kushindwa kuwa na mikakati ya maendeleo ya kuongoza vyama vyao.
Vipo vyama vya michezo ambavyo hata vikiulizwa ni kwa kiasi gani vimetekeleza dira ya maendeleo yake ya mwaka mzima kwa kipindi hiki cha mwisho wa mwaka majibu yatakuwa hasi.
Kwanza vyama hivyo unakuta havina hata mipango ya maendeleo ya kukuza michezo yao inayoiendesha na mwishoe kujikuta michezo husika inabakia kuwa na hali tete.
Vipo vyama vya michezo ambavyo havina akaunti au akaunti zake ni zile binafsi na hivyo kutoa wakati mgumu kwa wadhamini kuvisaidia.
Inatakiwa vyama vya michezo kubadilika na kujua hata bajeti za udhamini za wa makampuni mbalimbali ili kuandika maombi ya udhamini mapema. Pia viweke wazi ratiba nzima ya matukio yao kwa mwaka.
Ni jukumu sasa kwa waandishi wa habari kufuatilia vyama na kujua iwapo wanayo mikakati ya maendeleo ya mwaka mzima na inasemaje.
Iwapo aina hii ya ubabaishaji wa viongozi ikimalizwa ni dhahiri kuwa hata mwelekeo wa kukua kwa michezo nchini utakuwapo. Kuna vyama kama vile Chama Cha Riadha ambapo kuna viongozi waliokaa muda mrefu madarakani na kila kukicha vyama havina mafanikio.
Kukosekana mafanikio kwenye vyama vyao hivyo ndio chanzo cha kuanza kwa imani za kishirikina kama msingi wa maendelezo ya soka.
Kwa muda mrefu imani za kishirikina zimekuwa zikitumika kama tumaini la ushindi kwa wachezaji na washabiki wa timu husika hasa kwa timu kama za Simba na Yanga.
Frank Macha ni mdau wa soka ambae amekuwa meneja wa Uwanja wa Uhuru wa sasa ambao wakati huo ulikuwa ukiitwa Uwanja wa Taifa kwa awamu mbili ambapo alianza mwaka mwaka 1986 hadi 1997 na kisha akarejea mwaka 2000 hadi 2002.
Mdau huyo wa soka anaelezea namna ambavyo alikuwa akishuhudia matukio ya ajabu kuhusiana na imani hizo za kishirikina ambapo anatolea mfano wa kuzikwa kwa wanyama uwanjani pamoja na mengineo.
Anasema kuwa ilifika wakati alikuwa akilazimishwa na kamati za ufundi iwe za Yanga au Simba kuwaruhusu kuingia mapema ili timu ziweke ushirikina wao wakati wa mechi uwanjani hapo.
"Imani ya kama hizo za kishirikina zilikuwapo ila sijui kwa sasa hali ipo najua kwa sasa kuna huu uwanja mpya na unalindwa sana tu ila kwa miaka ile ilikuwa muda mwengine hata wakitumia njia waliozokuwa wakizijua wao na kufanikisha kufanya matukio hayo ya kishirikina."anasema.
Hata hivyo Amis Hemed ambae anadai kuwa aliwahi kuwa mlinzi katika uwanja wa Taifa wa zamani ambao kwa sasa ni Uhuru, anasema kuwa alikuwa akihongwa fedha ili kuruhusu watu kuingia kufanikisha matukio ya kishirikina kabla ya kuanza kwa mechi.
Masuala kama haya ndio yanarudisha nyuma maendeleo ya soka ambapo inatakiwa pia waandishi wa habari kuhakikisha kuwa wanakabiliana nayo.
Hii inatoa picha kuwa soka kwa hapa nchini limekuwa likiendeshwa kimizengwe kwa muda mrefu hasa kutokana na kuwa na viongozi wasio na mikakati ya ushindi na kuekeza uchawi kama njia ya kupata mafanikio katika michezo.
Bado waandishi wa habari wakichunguza na kupambana na rushwa,ubabaishaji na ushirikina kwa kuwaanika wahusika na uchafu kama huu inaweza kwa kiasi kikubwa kuleta mabadiliko na kuhakikisha maendeleo ya kweli kwenye soka.