Ifahamu mikakati ya wasanii kwa mwaka huu
http://habari5.blogspot.com/2014/01/ifahamu-mikakati-ya-wasanii-kwa-mwaka.html
Na mtaalamu wa masuala ya sanaa
KILA mwaka mpya unapoanza wadau mbalimbali wanakuwa na mikakati mbalimbali mipya ya kimaendeleo ikiwa pamoja na kukuza kazi zao au tasnia nzima kwa ujumla.
Kwa upande wa tasnia ya muziki pamoja na sanaa nzima kwa ujumla wadau mbalimbali wameelezea mikakati yao ua miaka ijayo.
Wasanii wakubwa mbalimbali wamegusia changamoto walizokutana nazo miaka iliyopita huku wakielezea yale wanayotaka kuyafanya kwa miaka ijayo.
Imezoeleka kuwa wasanii wakizungumzia mikakati mipya mara nyingi inakuwa ni kutunga na kuimba nyimbo mpya lakini hiyo imekuwa ni tofauti kwa baadhi ya wasanii waliozungumza na gazeti hili.
Msaii Dogo Janja kwa upande wake anasema kuwa amekuwa akijituma kufanya nyimbo nzuri kwa kila mwaka lakini anaona kuwa mwaka huu kipaumbelea chake akiweke mahala pengine.
Anasema kuwa kwa muda mrefu amekuwa ni mmoja kati ya wasanii wanaosikika kwa sana katika vyombo vya habari kwa kufanya nyimbo nzuri na mpya.
Lakini anasema kuwa kwa mwaka huu ana mpango wa kusisitiza zaidi suala zima la elimu.
Anasema kuwa kwake elimu ni kitu muhimu na hivyo ameamua kujiunga na masomo ya jioni katika kituo cha Ras Simba na kwa lengo la kuongeza uelewa.
"Kwa mwaka huu mimi naona kuwa kwangu shule ndio kitu cha msingi kwa sasa kwa kuwa bila shule sio kila kitu kitakuwa sawa, na lakini sina maana kuwa sitorekodi nyimbo mpya"anasema Dogo Janja.
Wazo kama hilo pia analo msanii Young Killer ambae anatamba na wimbo uitwao Dear Gambe, Miss Super Star na nyinginezo.
Msanii huyo anasema kuwa mbali na kupata fedha nyingi kwa njia za kufanya maonesho kadhaa nchini anaona kuwa shule ndio mahala pa kwanza kwake kuwekeza.
Anasema kuwa ana mpango wa kuendelea na kidato cha tano na sita ili kuongeza uelewa wa mambo utakaosaidia kazi zake za sanaa kukubalika zaidi.
"Muziki kwa sasa ni kazi na hivyo ili kazi ifanyike vema inatakiwa angalau kwa msani kuwa na shule ili kujiimarisha katika suala zima la mashairi na hata kusimamia kazi zangu mwenyewe"alisema Young Killer.
Mbali na kusoma wasanii wengine wameonesha nia ya kutaka kujiingiza kwenye aina nyingine ya sanaa.
Wapo wasanii wengine wa kama Tanzania ambao walikuwa wasanii wa filamu na wakajiingiza kwenye muziki na wakajikuta wakifanya vema zaidi.
Kama vile Shilole na hata Snura ambao kwa sasa ni gumzo mjini, ila kwa sasa pia wapo ambao wanafanya muziki na malengo yao kwa mwaka huu mpya unaoanza ni kuja kujiingiza kwenye filamu.
Tunda Man ni mmoja kati ya wasanii ambao wanauangalia mwaka huu ni kama mwaka wao wa kujiingiza kwenye filamu pia.
Tunda mana anasema kuwa anajiona kuwa yeye ni zaidi ya msanii kwa kuwa alijigundua kuwa anauwezo wa kucheza soka miaka mingi iliyopita na akafanya vema.
Alisema kuwa alifanikiwa kucheza hadi timu ya vijana ya Yanga kutokana na soka kabla ya kujigundua kuwa ana uwezo wa kuimba pia.
Anasema kuwa kama alivyoweza kufanya hivyo kuanzia kwenye kugundua kipaji chake cha kuimba kutoka kucheza soka ndio anavyoweza kufanya vema pia katika filamu.
Anaongeza kuwa anaiona fursa kubwa kwenye tasnia ya filamu ambayo anataka mwaka huu usipite bila ya kuitumia fursa hiyo kujiongezea kipato.
"Yah mimi kwa sasa ninataka kuhakikisha kuwa huu mwaka pia ninautumia kuigiza filamu na kutoka na kazi nzuri pia kwa kuwa hiyo ni moja kati ya njia za kujiongezea kipato pia"anasema Tunda Man.
Wazo kama hilo ndio anaonekana pia kuwa nalo msanii Rich Mavoko ambae kwa sasa anatamba na wimbo wa Roho Yangu.
Kwa upande wake anasema kuwa ana mpango wa kuweka kwenye filamu asilimia 80 ya yale anayoyaimba kwenye nyimbo zake.
Anasema kuwa ili kuhakikisha kuwa elimu inayokusudiwa kwenye nyimbo zake kuwafikia kirahisi wananchi ni vema wakaona matukio katika video.
"Kama wasanii jukumu letu kubwa ni kuwaelimisha wananchi kuhusiana masuala mbalimbali sasa kwa kulizingaita hilo nimeona kuwa nie vema niingie pia kwenye sanaa ya filamu"alisema Mavoko.
Kutokana na Tunda Man na Mavoko kuungalia mwaka huu kama ni mwaka wao filamu lakini pia wote wanaonekana kuwa bado wanania ya kuendelea na muziki pia.
Wapo wasanii ambao wanaona kuwa ni vema wakaendelea na sanaa zao hizo hizo ila wanachofanya ni kubadilisha mikakati ya ufanyakazi kazi.
Ambwene Yesaya anaona kuwa ni mwaka wake wa kurudisha kidogo katika jamii kwa kuwasaidia wasanii wasiokuwa na majina au wageni kabisa.
Ay alisema kuwa amepata vipaji viwili ambavyo anataka kuvikuza katika kampuni yake ya Unity Entertainment ambayo inashugulikia masuala ya kukuza vipaji vya wasanii wa muziki.
Anasema kuwa akianza kwa namna hiyo kwake anaona kuwa anatimiza majukumu makubwa ya kuinua maisha ya vijana wenzake katika sanaa.
"Sanaa kwangu imekuwa ni ajira rasmi ambayo imenisaidia kwa kiasi kikubwa katika maisha yangu, sasa ni kwa nini nisifurahi kuona ikiwasaidia wengine pia"alihoji AY.
Anaongeza kuwa mwaka 2014 kwake ni mwaka ambao anataka kuutumia tofauti huku lengo lake kubwa likiwa ni kuhakikisha kuwa analeta mabadiliko katika sanaa kwa kusaidia vijana.
Wasanii ni vema mkautazama mwaka huu 2014 kuwa ni wa mabadiliko ya kikazi yenye tija kipato.