Yanga yatua Uturuki kwa ajili ya mazoezi
http://habari5.blogspot.com/2014/01/yanga-yatua-uturuki-kwa-ajili-ya-mazoezi.html
TIMU ya Yanga iliondoka jana ikiwa na msafara wa wa watu 33 wakiwemo wachezaji 27 kuelekea nchini Uturuki kwa shirika la ndege la Uturki (Turkish Airlines) kwa lengo la kuweka kambi ya mafunzo kwa muda wa takribani wiki mbili kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom pamoja na mashindano ya kimataifa.
Yanga imefikia katika hoteli ya kitalii ya Sueno Beach Side iliyopo km 70 kutoka katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Antalya ikiwa katika eneo la ufukwe na mji wa kihistoria Magnavat.
Hii inakua ni mara ya pili mfululizo kwa timu ya Young Africans kwenda kuweka kambi katika jiji la Antalya ambapo msimu uliopita pia iliweza kuweka kambi katika mji huo, kambi ambayo ilikuwa na mafanikio makubwa baada ya kurejea nchini kwani timu iliweza kucheza mzunguko wa pili pasipo kupoteza mchezo hata mmoja mpaka ilipotwaa Ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom.
Walioondoka na timu hiyo ni pamoja na kocha msaidizi Charles Boniface Mkwasa na kocha wa makipa Juma Pondamali ambao wataendelea na mafunzo nchini Uturuki wakati uongozi unaendelea na mchakato wa kumpata kocha mkuu ambaye ataungana na kikosi hicho.
Mkuu wa msafara huo ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Salim Rupia ambaye ataongozana na msafara huo kwa kipindi chote cha wiki mbili mpaka kikosi kitakporejea nchini Januari 23 mwaka huu tayari kwa kmzunguko wa pili.
Watu wengine walioongoza na timu ni pamoja na Baraka Kizuguto ambae ni Afisa Habari, Charles Mkwasa ambae ni Kocha msaidizi, Juma Pondamali ambae ni Kocha wa Makipa, Suphian Juma ambae ni Daktari wa timu na Hafidh Salehe ambae ni Meneja wa timu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyowekwa kwenye tovuti ya klabu hiyo inaongeza kuwa walinda mlango wlaiosafiri na timu hiyo ni pamoja na Juma Kaseja, Ally Mustafa "Barthez" na Deogratias Munish "Dida"
Walinzi waliosafiri na timu hiyo ni pamoja na Mbuyu Twite, Juma Abdul, David Luhende, Nadir Haroub "Cannavaro", Kelvin Yondani, Oscar Joshua, Ibrahim Job na Rajab Zahir.
Katika nafasi ya viungo walioongozana na timu ni pamoja na Frank Domayo, Hasssan Dilunga, Haruna Niyonzima, Nizar Kahlfani, Hamis Thabit na Bakari Msoud
Kwa upande wa washabuliaji walioondoka ni pamoja na Didier Kavumbagu, Hamis Kiiza, Emmanuel Okwi, Hussein Javu, Said Bahanuzi, Jerson Tegete, Mrisho Ngasa, Saimon Msuva, Shaban Kondo na Reliants Lusajo
ends