Mdau wa Chadema aliepewa kipigo aruhusiwa kutoka hospitali
http://habari5.blogspot.com/2014/01/mdau-wa-chadema-aliepewa-kipigo.html
HALI ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Joseph Yona, imeelezwa kuendelea vizuri hali iliyofanya aruhusiwe kutoka hospitali.
Taarifa za Yona kutoka hospitalini zimetolewa jana na Msemaji wa Taasisi ya Mifupa, Mishipa ya Fahamu na Upasuaji wa Ubongo (MOI), Jumaa Almasi wakati akizungumza na gazeti hili jana ofisini kwake.
Yona alifikishwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili juzi, baada ya kupatika akiwa na majeraha ambayo anadai alitekwa nyara na kupigwa mpaka kupoteza fahamu.
Almasi alisema baada ya kufanyiwa vipimo na kupewa matibabu Mwenyekiti huyo aliruhusiwa kwa kuwa hali yake ilikuwa ikionyesha alikuwa anaendelea vizuri.