Fresh Prince azidi kumlilia mjomba wake
http://habari5.blogspot.com/2014/01/fresh-prince-azidi-kumlilia-mjomba-wake.html
MWIGIZAJI mahiri wa Filamu,Mchekeshaji pamoja na Mwanamuziki mahiri wa Marekani Will Smith,Fresh Prince ameonesha kusikitishwa na kifo cha mlezi wake katika sanaa James Avery.
Avery alikuwa akijulikana kama Phillip Banks katika tamthilia ya The Fresh Prince of Bel-Air alifariki ,hivi majuzi akiwa na miaka 68.
Katika tamthilia hiyo Avery alikuwa akiigiza kama mjomba wa Fresh Prince.
Fresh Prince alisema kuwa ameguswa na kifo hicho hasa kutokana na nafasi ya mwigizaji mwenzeke huyo katika kukuza sanaa yake.
Alisema kuwa amekuwa akijifunza mengi kutoka kwake na hadi anapoteza maisha alikuwa bado kuna mengi anaendelea kujifunza.
Hadi anapoteza maisha Avery alikuwa anaendelea kushiriki kwenye tamthilia kama vile Grey's Anatomy na filamu mbalimbali.
Pia kifo hicho kimemgusa mke wa Fresh Prince Jada Pinkett Smith ambae nae alisema kuwa msiba huo ni mkubwa sio tu kwake na kwa mumewe Fresh Prince bali kwa tasnia nzima ya sanaa.