Mgimwa aagwa rasmi, Pinda aongoza maziko Iringa
http://habari5.blogspot.com/2014/01/mgimwa-aagwa-rasmi-pinda-aongoza-maziko.html
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amewasili mjini Iringa leo asubuhina kwenda kijiji cha Magunga tarafa ya Kiponzelo wilayani
Iringa, kukagua maandalizi kwa ajili ya mazishi ya aliyekuwa Waziri wa
Fedha, Dk. William Mgimwa. Anatarajiwa kuzikwa nyumbani kwake kwenye
makaburi ya familia.
Waziri Mkuu amewasili Iringia akitokea kijijini kwake Kibaoni, wilayani
Mpanda, Katavi alikokuwa ameenda kwa mapumziko ya mwisho ya mwaka.
Mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Nduli na kupokewa na viongozi wa
mkoa wa Chama na Serikali, Waziri Mkuu alikwenda kijiji alichozaliwa Dk.
Mgimwa cha Magunga ambacho kipo kilometa 66 kutoka Iringa mjini.
Akiwa kijijini hapo Waziri Mkuu Pinda aliwapa pole mama mzazi wa Dk.
Mgimwa, Bibi. Consolata Semgovano pamoja na wajomba zake wakiwemo na wafiwa
wengine. Pia alikagua kazi ya ujenzi wa kaburi atakamozikwa hapo kesho,
uwekaji wa mahema pamoja na eneo la kufanyia ibada ya mazishi. Vilevile
alikagua mahali ambapo mwili wa marehemu utalazwa usiku huu ukisubiri
taratibu za mazishi hapo kesho.
Waziri Mkuu amerejea mjini Iringa ili kuusibiri mwili wa Dk. Mgimwa ambao
unatarajiwa kuwasili uwanja wa ndege wa Nduli leo jioni na kwenda kuagwa na
wakazi wa Iringa kwenye ukumbi wa ‘Siasa ni Kilimo’ kisha utapelekwa
kijijini kwao Magunga ambako utalala nyumbani kwake.
Dk. Mgimwa alifariki dunia Januari mosi, mwaka huuakiwa Afrika Kusini
ambako alikuwa akipatiwa matibabu. Ameacha mjane na watoto saba, wawili wa
kike na watano wa kiume.