Vodacom yamuunga mkono Waziri wa Michezo Fenella Mukangara katika ligi ya shule za Sekondari

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mh. Dk. Fenella Mukangara (wa kwanza kushoto)  na Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom (wa pili kushoto), Salum Mwalim ambao ndio wadhamini wa vifaa hivyo wakikabidhi vifaa vya michezo kwa mwanafunzi wa shule ya sekondari Mnazi Mmoja, Shaha Bakari (wa kwanza kulia) kwa ajili ya mashindano yatakayo husisha shule za sekondari Dar es Salaam. Wa pili kutoka kushoto ni Mwalimu wa shule hiyo, Alex Dumien akishuhudia makabidhiano hayo, michuano hiyo itahusisha shule za sekondari kumi na mbili, nne kutoka kila wilaya ya mkoa wa Dar es Salaam.
Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom (wa kwanza kushoto), Salum Mwalim ambao ndio wadhamini wa vifaa hivyo wakikabidhi vifaa vya michezo akikabidhi mfano wa hundi ya milioni moja kwa katibu mkuu wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Henri Lihaya (wa pili kushoto) fedha ambayo itatumika katika mashindano yatakayohusisha shule za sekondari za Mkoa wa Dar es Salaam. Wa pili kushoto ni  Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mh. Dk. Fenella Mukangara na Naibu Katibu Mkuu wake, Prof. Elisante Ole Gabriel (wa kwanza kulia) wakishuhudia makabidhiano hayo.
Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom (wa kwanza kushoto), Salum Mwalim ambao ndio wadhamini wa vifaa hivyo wakikabidhi vifaa vya michezo akikabidhi mfano wa hundi ya milioni moja kwa katibu mkuu wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Henri Lihaya (wa pili kushoto) fedha ambayo itatumika katika mashindano yatakayohusisha shule za sekondari za Mkoa wa Dar es Salaam. Wa pili kushoto ni  Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mh. Dk. Fenella Mukangara na Naibu Katibu Mkuu wake, Prof. Elisante Ole Gabriel (wa kwanza kulia) wakishuhudia makabidhiano hayo.   
Habari Kamili
WAZIRI wa Wizara ya Habari,Utamadun, Vijana na Michezo Fennela Mukangara jana alikabidhi vifaa vya michezo kwa shule za sekondari 12 zitakazoshiriki ligi ya Dar es salaam Community Sports Cup.

Ligi hiyo maalum kwa ajili ya kuandaa wanamichezo bora wa baadae itaanza Februali 8 mwaka huu na kushirikisha sekondari zilizopo wilaya ya Ilala, Kinondoni na Temeke chini ya udhamini wa kampuni ya simu ya mkononi ya Vodacom n aimehasisiwa na waziri huyo.


Akizungumza kabla ya makabidhiano hayo, Mukangara alisema kuwa michezo ni biashara kamii ambayo inapaswa kuwekezwa kwa ajili ya manufaa ya baadae.


Alisema kuwa ili kuwa na ligi bora ya baadae ni vema maandalizi yakaanzia kwa sasa tena katika kuwandaa wanafunzi tangia wakiwa shuleni.


Alisema kuwa kilichomsukuma kuhasisi Ligi hiyo ni kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa na wanamichezo imara wa baadae wenye kuwa na misingi mizuri  ya michezo.


Alisema kuwa kwa sasa mradi huo uliopo kwenye majaribio umeanza na mchezo wa soka lakini kwa baadae itahamia katika michezo mingine kama vile Netiboli na mingineo.


Pia aliwataka Maofisa Tawala wa Mikoa kuhakikisha kuwa wanakuwa na maandalizi mapema ya kuziandaa sekondari kushiriki ligi kama hiyo ambayo baadae itafika hadi mikoani.


"Nawaagiza Maofisa Tawala wa Mikoa kuhakikisha kuwa wanajipanga ili pindi ligi hii itakapofika mikoani mwao waweze kuiendesha pia"alisema Mukangara.


Meneja Mawasiliano wa nje wa Vodacom, Salum Mwalimu alisema kuwa kampuni hiyo imeridhishwa na michezo hiyo na kuamua kudhamini vifaa vya michezo.


Vodacom ilitoa mipira, viatu, kombe na vifaa vingine muhimu vya michezo kwa wanafunzi hao.


Kwa upande wake msimamizi wa Ligi hiyo kutoka Sekondari ya Kibasila, Abel Mtweve alisema kuwa katika shule 12 zinazoshiriki ligi zitakuwa zikicheza kila siku ya Jumamosi na Jumapili katika wilaya zao.


Alisema kuwa katika mechi mbilimbili zitakazokuwa zikichezwa na timu hizo washindi kutoka kila wilaya watakutana katika ngazi ya nusu robo fainali, nusu fainali na kisha fainali.


Alisema kuwa kwa wilaya ya Temeke kituo kitakuwa katika sekondari ya Kibasila, huku wilaya ya Ilala itakuwa ni Sekondari ya Benjamini Mkapa na kisha Kinondoni itakuwa ni Sekondari ya Tuliani.
 

Meneja wa Mahusiano wa nje wa Vodacom, Salum Mwalim alisema kuwa Vodacom itaendelea na harakati za kusaidia masuala ya elimu kwa ngazi zote kuanzia Msingi, Sekondari na kuendelea.

Alisema kuwa inatambua nafasi ya michezo shuleni kwa kuwa ndio msingi imara wa kuinua vipaji.

Maoni yangu
Naipongeza sana Vodacom kwa kazi yake nzuri ya kuangalia michezo katika ngazi hiyo na inatakiwa harakati kama hizi kuungwa mkono na wadau wengine hasa makampuni ya simu. 
Mwisho

Related

Sticky 4921037758196691607

Post a Comment

emo-but-icon

item