Lupita na Brad Pit mh!!!

MCHEZA filamu mwenye asili ya Kenya Lupita Nyong’o (31) anaetamba kwa sasa nchini Marekani amekiri kuwa kwa sasa wanaume wengi wamekuwa wakimfata na kutaka kuwa nae.

Kwa sasa Kenya kumekuwa na tetesi kuwa ndoa ya wacheza filamu wapenzi Lizz Nyagah and Alex
Konstantaras ipio mashakani kutokana na Alex kuwa na uhusiana na Lupita.

Inagwaje tetesi hizo zimepingwa vikali na Lizz na kusisitiza kuwa Lupita hana uhusiano na mumewe huyo.

Kwa upande wa Hollywood, uhusianao kati ya Angelina na mumewe Brad Pitt umekuwa mashakani kutokana na kuwepo kwa tetesi kuwa Lupita anatoka na Brad Pitt.

Tetesi kuhusiana na uhusiano kati ya wawili hao ziliibuka zaidi pale ambapo Brad Pitt wakati wa utoaji wa tuzo za Producer Guild alijikuta akitoa maneno matamu kuhusiana na Lupita ambayo vyombo vya habari vilitafsiri tofauti.

Brad Pitt alisema kuwa Lupita ni mwanadada ambae ni muhimu sana na kuongeza kuwa kuna mengi mazuri na matamu yanakuja kutoka kwake.

Kauli hiyo ilionekana kutomfurahisha Angelina ambae pindi waliporejea nyumbani hakuwa na furaha kutokana na kauli hiyo ya Brad Pit.

Taarifa zinadai kuwa kwa upande wa Angeli Jolie alimkaripia mumewe huyo kwa kusisitiza kuwa hakuwa na sababu ya kumsifia Lupita kwa kiasi kikubwa namna.

 Alisema kuwa anatakiwa kutambua kuwa yeye ni kama mume wa mtu na sio kina mhuni na kitendo kama kile ni kitendo cha kihuni kumsifia mwanamke mwengine.

Inasemekana kuwa wakati wa utoaji wa tuzo hizo Brad Pitt na Lupita Nyong’o walikuwa karibu muda wote.
Pia hata wakati mwigizaji mwengine Leonardo DiCaprio alipotokea na kumbusu Lupita Brad Pit alionekana kukasirika na kutoa kauli ya utani akimwambia DiCaprio kuwa mbali na mwanadada huyo.

Hali hiyo ndio inawafanya wachambuzi wa mambo kuhisi kuwa huenda Brad Pit akamshirikisha tena katika filamu nyingine.
==========================================

Related

Sticky 8019711654905337008

Post a Comment

emo-but-icon

item