Yanga kurudi Alhamis hii ya January 23


KIKOSI kizima cha timu ya Yanga kinatarajia kurejea hapa nchini keshokutwa kikitokea Uturuki kilipokuwa kimeweka kambi.


Kikosi hicho kinarejea hapa nchini ikiwa ni siku mbili kabla ya kuanza kwa mzunguko wa pili wa ligi kuu itakayoanza Januari 25 mwaka huu.


Akizungumza na gazeti hili Katibu Mkuu wa Yanga Bernard Njovu alisema kuwa kikosi hicho kipo katika haki nzuri na kimejiandaa vema na mzunguko huu wa pili.


Alisema kuwa wachezaji, viongozi na msafara mzima wa timu hiyo unaendelea vema na kipo tayari kwa ushindi.


"Kma mnavyojua kuwa tarahe 23 ndio safari ya mzunguko wa pili wa ligi kuu inaanza na timu yetu itawasili hapa nchini siku hiyo tayari kabisa kwa kutetea kombe letu"alisema Njovu.


Yanga imetumia muda wake wa mapumziko kujifua Uturuki chini ya kocha wao   Hans van der Pluijm.


Ikiwa Uturuki Yanga imecheza mechi kadhaa za kirafiki kujiandaa na awamu hiyo ya pili ya ligi.


Mecho nyingi ilizocheza na timu za Uturuki Yanga imeonekana kufanya vema dalili ambayo inaashiria kuwa kambi hiyo ya mazoezi kwa timu hiyo ilikuwa ni ya faida.


Katika hatua wajumbe wa mkutano mkuu wa Yanga wameonesha nia yao ya kumrudishia mchezaji wa timu hiyo Mrisho Ngasa Milioni 45 alizoilipa klabu ya Simba.


Ngasa alitakiwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuilipa klabu ya Simba Milioni 45 ili kuwa huru zaidi kuitumikia klabu ya Yanga.


Akizungumza kwa niaba ya wanachama wenzake  Mwenyekiti wa Yanga tawi la Buguruni, Mshana Waziri alisema kuwa wanachama hao wanajichangisha fedha zao pamoja wanachama wengine ili kumrejeshea Ngasa Milioni 45 zake.


"Tunajua kuwa Ngasa ni mchezjai wetu wa muda mrefu akiwa anaitumikia klabu hii na tunataka kuhakikisha kuwa ule mzigo aliojitwisha wa kuilipa Simba sisi tunayapunguza machungu yale"alisema Mshana.


Yanga kwa sasa ndio inashirikia Kombe la Ligi Kuu Tanzania bara.

Related

Sticky 2393569805809193122

Post a Comment

emo-but-icon

item