RT yataka wadau kuguswa na hotuba ya JK
http://habari5.blogspot.com/2014/01/rt-yataka-wadau-kuguswa-na-hotuba-ya-jk.html
CHAMA Cha Riadha Tanzania, RT kimesema kuwa kimepokea kwa msisimko mkubwa hotuba ya Rais Jakaya Kikwete aliyoitoa kuhusiana na chama hicho wakati akipokea kifimbo cha Malkia katika viwanja vya Ikulu juzi.
Juzi Raisi katika hotuba yake hiyo aliwataka viongozi wa RT kuwa na mikakati endelevu itakayosaidia kuendeleza mchezo wa riadha nchini.
Alisema kuwa viongozi wa RT wamekuwa wakichelewa kuandaa timu na kuanza maandalizi yao ikiwa ni siku chache kabla ya kuanza kwa michezo husika.
Akizungumzia hotuba hiyo Rais wa RT Anthony Mtaka alisema kuwa kwa upande wa chama hicho wameipokea hotuba hiyo kwa mikono miwili na imetoa mwanga kwa mustakaballi wa chama hicho.
Alisema kuwa ni hotuba ambayo mbali na kukichambua chama cha RT lakini pia ni wakati muafaka kwa wale ambao wameombwa msaada na chama hicho kuanza mchakato wa kukisaidia.
Alisema kuwa chama cha RT kinahitaji fedha kwa ajili ya maandalizi ya timu ya Taifa ya riadha ambapo shilingi milioni 300 zinahitajika.
Alisema kuwa kwa sasa mchanganuo mzima wa namna ambavyo fedha hizo zitatumika upo kwenye Wizara ya Habari, Vijana, Utamadunia na Michezo na wanasubiria fedha ili waanze kazi.
Alisema kuwa tayari mchakato wa kutafuta wachezaji watakaoshiriki michuano hiyo ya Jumuia ya Madola imeshakamilika na kwa sasa kinachosubiriwa kwa sasa ni kuanza kwa kambi.
Alisema kuwa Februari 9 kutakuwa na kikao cha awali cha kujadiliana uendeshai wa kambi hiyo itakayofanyika Hombolo Dodoma.
Alisema kuwa wanariadha hao wataweka kambi hiyo katika chuo cha Serikali za Mitaa kilichopo katika eneo hilo la Hombolo lakini kwa baadae watahamia Babati.
Alisema kuwa mikakati yote hiyo ili kufanikiwa inahitaji fedha na akaongeza kuwa kwa kupitia hotuba ya Rais Kikwete wadhamini wajitokeze na pia kwa wale ambao wanatakiwa kutimiza majukumu kwa upande wao wafanya hivyo.
"Sisi kazi yetu ni kuandaa timu ambapo tayari tumeshaifanya na kwa sasa ni upande wa pili ambao ni wa kusaidiwa kufanikisha kambi hii , msaada ambao kila mdau anakuwa na jukumu lake la kutimiza na kwa sasa naona kuwa ni vema hilo likafanyika"alisema Mtaka.
Aliongeza kuwa wamepata wachezaji kutoka katika Jeshi la Polis, Jeshi la Wananchi, Sekondari, na wachezaji wa timu za taifa waliopita.
Alisema kuwa katika hotuba ya Rais ambapo alisisitiza kuwa maandalizi ya timu hiyo ni muhimu na inatakiwa yafanyike mapema kwa upande wake anaona kuwa RT imeshafanya maandalizi yake na hivyo anaomba upande wa pili wa msaada utakaofanikisha kambi utimizwe mapema ili kambi ianze mapema.
Julai 23 ndio siku ambayo inatakiwa kuanza kwa michezo hiyo ya Jumuia ya Madola hadi Agosti 3 mwaka huu.