Hebu pata kuyasikia haya kutoka kwa kundi la Tamthilia la Mahusiano
http://habari5.blogspot.com/2014/02/hebu-pata-kuyasikia-haya-kutoka-kwa.html
Wasanii wa kundi la Mahusiano wakiwa pamoja na Wadau wa sanaa |
Hii ni picha kutoka maktaba ya blog hii |
Na Mwandishi wa Blog hii
KUNDI la Mahusiano ni moja kati ya makundi yanayokuja kwa kasi kubwa hapa nchini katika tasnia ya maigizo.
Mchezo wa kundi hilo unarushwa katika kituo cha Luninga cha Clouds Tv ni moja kati ya michezo ya Luninga inayotazamwa zaidi kwa sasa.
Ni mchezo unaozungumzia maisha ya kila siku katika mahusiano yawe ya ndoa au mahusiano ya wapenzi wa kawaida.
Akizungumza na safu hii msemaji wa kundi hilo, Rachel Kuyunga ambae anaigiza kama mke wa Mwinjaku katika mchezo huo alisema kuwa lengo la mchezo huo ni kuonesha yake yanayotokea katika jamii.
Alisema kuwa katika jamii ya sasa kuna wanawake wengi wanakumbwa na kero mbalimbali katika mahusiano yao na wanashindwa kujua namna bora ya kukabiliana nayo na ndio mcheozhuo unatoa suluhu ya hayo yote.
Alisema kuwa katika kuhakikisha kuwa ujumbe mzima unawafikia wananchi wamejipanga kuhakikisha kuwa wanafanya maonesho ya jukwaani.
"Kwa sasa tunaendelea na kuelimisha jamii kupitia maigizo hayo yanayooneshwa kwenye Luninga ila kwa muda ukifika tutaingia kwenye live Performance na hapo ndipo pia utakuwa mwanya wa kuonesha ukali wetu zaidi"alisema Rachel.
Wasanii wengine wanaotamba katika igizo hilo ni Aika Steven, Charles Mwendo, Davis Ng'indu, Mariam Rashid, Mwemba Burton, Neema Mbuya na Farida.