Vanessa ayataka makampuni kuandaa shoo za wazi nyingi
http://habari5.blogspot.com/2014/02/vanessa-ayataka-makampuni-kuandaa-shoo.html
MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Vanessa Mdee ameyataka makampuni mbalimbali kujitokeza na kuandaa matamasha ya wazi.
Vanessa alisema kuwa matamasha ya wazi yanarahisisha wasanii kukutana na washabiki wao kirahisi zaidi.
Alisema kuwa kwa kuwa katika matamasha hayo ya wazi wananchi wanapata burudani ya bure hivyo wengi wao wanaingia kwa wingi na kukutana na wasanii hao.
Alisema kuwa watu wengi wanapenda kuwaona wasanii wakubwa wakiburudisha lakini wanashindwa kufanya hivyo kutokana na kukwazwa na viingilio.
Alisema kuwa pia wapo wanafunzi ambao wanabanwa na mazingira na hivyo kushindwa kuwaona wasanii hao wakiimba hivyo kwa shoo hizo za wazi zinawasaidia kwa upande wao.
Alisema kuwa makampuni yakishiriki katika kuandaa shoo za wazi wanakuwa wamewavutia kwa kiasi kikubwa washabiki wengi wenye kushindwa kuhudhuria shoo zao za kila siku.
"Ni vema makampuni yanayoandaa shoo kama hizi za wazi kuendelea kufanya hivyo kwa kuwa ndio njia ya kuwawezesha watanzania wa kawaida kuwa nasi pamoja lakini pia hata na sisi wasanii tunapata fedha nzuri kwa kiasi fulani"alisema Vanessa.