Juma Nature asisitiza kutobadilisha aina yake ya ya muziki
http://habari5.blogspot.com/2014/02/juma-nature-sitobadilisha-aina-yanguya.html
MSANII mkongwe kwenye muziki wa kizazi kipya hapa nchini, Juma Nature amesema kuwa ataendeleza aina yake ya uimbaji kwa miaka yote.
Juma Nature alisema kuwa akiwa kama msani mkongwe amewaona wasanii wengi wapya wanaokuja na kuimba kwa staili zao tofauti.
Alisema kuwa kwa upande wake ataendelea na nyimbo zake za aina hiyo hiyo alizozizoea na kusisitiza kuwa hatoimba kama wauza sura wengine.
"Mimi muziki ni kazi na nawakilisha watu wangu wa maeneo mbalimbali kwa staili yangu ya kikazi zaidi na sio kuuza sura, sasa kama ngoma yangu ya sasa ukiisikiliza ni kama ngoma ile ile ya miaka ya nyuma"alisema Juma Nature.
Kwa sasa msanii huyo ana wimbo wake unaitwa Kama Jana ambao anazungumzia nyimbo zake za zamani na za sasa.
Safu hii ilipoufuatilia wimbo huo kuna sehemu anasikika akiimba kwa kusema kuwa Wewe dada mondi ukiitwa na mashabiki unalinga na muziki sio kukata viuno.
Alipulizwa kuhusiana na ujumbe huo alisema kuwa hana maana ya kumsema Diamond ila ni vipengele tu vya wimbo.
Hoja.
Hongera Nature kwa kuwa katika muziki kwa muda mrefu lakini unatakiwa kubadilika sasa na kuachana na aina hiyo ya mawazo.
Sina maana ya kuwa ni lazima ubadilike katika muziki wako ambao ndio kama utambulisho wako ila ninamaana kuwa kubadilika kimwenendo na kutoka katika usela zaidi na kuwa katika angalau usasa.
Hivi kwanza unayo hata Facebook Page manake kwa vile ulivyokuwa na mashabiki wengi ungetakiwa kuwa hata na Fan Page kabisa ili angalau kuwa karibu zaidi na washabiki wako.
Ila kwa vile unavyoendelea na usela muziki wa sasa sio kama ule wa miaka ile ulivyokuwa na washabiki wako wale ambao nakumbuka kwenye miaka ya 2001 hadi 2005 washabiki wako walikuwa wakikupenda zaidi kwa usela wako kama ule.
Ila kwa sasa tunaongelea miaka takribani 12 hivi na washabiki wapya wanakuja kwa maana ya kuwa kuna wapenzi wapya wa muziki ambao hiki sio tena kizazicha usela hiki inabidi nacho uendane nacho kisasa zaidi.
Ninamaana kuwa angalau badilisha mwonekano na kuwa katika mtazamo wa kimvuto zaidi kuanzia kuvaa, kuongea na hata kuwa na swaga ambazo zitakuvutia na kukuweka kuwa kama msanii wa kisasa.
Hiyo itaendana na video bora zaidi na hivyo kujikuta hata ukitoa wimbo mpya basi wapo watakaoununua zaidi na tena kujikuta ukiingiza fedha kwa njia ya Ring Tones.
Nature badilika bwana si unaona wenzako kama akina Diamond, Shetah, au hata akina Jux wamekukuta na kwa sasa wanaweza kuwa na washabiki sana na kukuacha mbali hiiinatokana na kuwa wanaendana na kizazi cha sasa chenye kununua nyimbo hata kwa Ringtone sio cha usela kama ule wa miaka ile ulivyokuwa ukiimba ambacho sijui hata kama wanaweza kukuunga mkono nyimbo zako zaidi ya kuzisikia na kuzisifia tu.
===============