Jokate bwana!!! hana hiyana na mtu
http://habari5.blogspot.com/2014/02/jokate-bwana-hana-hiyana-na-mtu_4.html
Huyu ndio Jokate Mwegilo ambae juzi alijiachia akiwa na Wema Sepetu jukwaani katika kumbi ya Triple A, Arusha. Jokate aliwahi kumchukulia Wema Diamond kipindi fulani. |
Hapa akiwa na Wopler ambae pia aliwahi nae kuwa na Diamond |
MWANAMITINDO, msanii na mwigizaji wa filamu Jokate Mwegilo amesema kuwa uamuzi wake wa kumfuata msanii Wema Sepetu jukwaani na kucheza nae muziki alilenga kuonesha jamii kuwa hana uhasama na msnaii huyo.
Jokate na Wema miaka ya nyuma walionekana kutofautiana hasa pale ambapo Wema aliibuka kuwa Miss Tanzania mwaka 2006 na kisha Jokate kushika nafasi ya pili.
Pia Jokate alikuja kuwa na uhusiano wa muda mfupi na msanii gwiji wa muziki wa Bongo Flavor, Nasib Abdul maarufu kama Diamond wakati huo msanii huyo alikuwa ni mpenzi wa Wema.
Hali hiyo ilipelekea watu wengi kuhisi kuwa watu hao wana uhasama wa muda mrefu lakini hata hivyo kwa hatua ya Jokate kwenda kucheza jukwaani na Wema iliashiria kuwa wawili hao wanaelewana na hawana ugomvi.
Jokate aliiambia safu hii kuwa anampenda Wema kwa kuwa ni msanii ambae ana uwezo wa hali ya juu katika kuigiza na kwa kuwa yeye kwa sasa ameanza kuigiza filamu anaona kuwa Wema ni msaada mkubwa kwake.
Alisema kuwa muda umefika kwake kusimama kama msanii kamili wa filamu na anaona kuwa msaada mkubwa kwake ni Wema kwa upande wa wanawake na pia anajipanga kufanya nae kazi za sanaa