Saidieni mchezo wa chess == Dk Mukangara

WADHAMINI mbalimbali wametakiwa kujitokeza kuudhamini mchezo wa Chess ili uweze kuchezwa katika shule za msingi na sekondari kama njia ya kujiimarisha kimasomo.
Wito huo ulitolewa juzi na Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Fenela Mukangara wakati alipokuwa akizungumza kama mgeni rasmi kwenye hafla ya uzinduzi wa mchezo huo hapa nchini.
Pia hafla hiyo ilihudhuriwa na Bingwa wa zamani wa mchezo wa chess ambae pia ni mmiliki wa Taasisi ya Kasparov Chess.
Fennela alisema kuwa kutokana ambazo mchezo huo imekuwa ikipatiwa kuwa unasaidia kuimarisha uelewa wa wanafunzi shuleni, hivyo ni vema hata hapa ncini ukatumiwa katika shule mbalimbali.
Alisema kuwa kwa upande wake yupo tayari kusaidia maendeleo ya mchezo huo hapa nchini kwa kuwa ni moja kati ya michezo ya ndani ambayo inahitaji kutangazwa hapa nchini.
"Chess ni mchezo wa aina yake ambao kumbe ukitiliwa mkazo unaweza kuleta mabadiliko katika elimu nchini kwa maana kuwa wanafunzi wanaweza kuucheza na hivyo kujikuta pia wakijiimarisha zaidi kiuelewa"alisema Mukangara.

Pia Waziri Fenella alimwomba Kasparov kupitia Taasisi yake kuendeleza mchezo huo hapa nchini.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Cha Chess Tanzania, Geoffrey Mwanyika alisema kuwa tayari chama hicho kimekubaliana na sekondari ya Shaban Robert kuanza kujifunza mchezo huo.
Alisema kuwa chama hicho katika kuhakikisha kuwa mchezo huo unafundishika katika shule nyingi hapa nchini kimeanza utaratibu wa kuwafundisha watu mbalimbali watakaokuwa na jukumu la kuwafundisha wanafunzi shuleni.
Alisema kuwa ili kufanikisha adhma hiyo kuna kila sababu ya wadhamini mbalimbali kujitokeza kudhamini jitihada za chama hicho katika kuuendeleza mchezo huo.
"Ili kutimiza ndoto zetu peke yetu hatuwezi kabisa hivyo basi ni vema wadau mbalimbali wakatuunga mkono katika jitihada zetu hizi kwa kuwa kwanza seti moja ya mchezo huo sio chini ya dola 5, na tunahitaji kuwa na vifaa hivi vingi"alisema Mwanyika.
Mwisho 

Related

Sticky 6400118223505637117

Post a Comment

emo-but-icon

item