Zantel ilivyonogesha mashindano ya Ngalawa Tanga


 Baadhi ya Ngalawa zilizoshiriki mashindano ya Ngalawa mwishoni mwa wiki hii mkoani  Tanga kwa udhamini wa Zantel
1.    Baadhi ya wananchi wakishuhudia mashindano ya Ngalawa yaliyofanyika mkoani Tanga kwa udhamini wa Zantel mwishoni mwa wiki hii.
Baadhi ya Ngalawa zilizoshiriki mashindano ya Ngalawa mwishoni mwa wiki hii mkoani  Tanga kwa udhamini wa Zantel.
Kampuni ya simu za mkononi  Zantel imepongezwa na wadau wa michezo kwa kudhamini mashindano ya Ngarawa  yaliyofanyika mwishoni mwa wiki hii mkoani Tanga katika kijiji cha Kigombe wilayani Muheza.

Mashindano hayo ambayo hufanyika kila mwaka kuenzi utamaduni wa maeneo ya mwambao wa pwani kwa mwaka huu yalijumuisha washiriki 150 kutoka wilaya tofauti ikiwa na zaidi ya timu 30 ambapo Juma Mgeni alitangazwa mshindi.


Wakizungumza baada ya kutangazwa kwa washindi, washiriki wengi waliipongeza Zantel kwa kuthamini michezo ambayo imesahaulika na wengi kama Ngarawa.


‘Wadhamini wengi hupenda kuchagua michezo ambayo ni maarufu tayari huku wakisahau michezo mingine kama ngarawa, bao na kadhalika’ alisema mgeni rasmi wa mashindano hayo, Amina Mwidau, ambaye ni mbunge wa viti maalumu.


Akizungumzia udhamini wa mashindano hayo, Afsa Biashara Mkuu wa Zantel, Sajid Khan alisema kampuni yake imeamua kufadhili mashindano ya Ngarawa mwaka huu kwa kuwa imebaini mchezo huo mbali na kutoa burudani, vile vile inaweza tumika  kama sehemu ya  kuibua vipaji vipya.


“Zantel itaendelea kuungana na jamii katika kudumisha na kukuza sanaa, kuhamasiha ubunifu na kuibua vipaji katika nyanja mbalimbali, ili kutoa nafasi kwa vijana kutumia ubunifu huo katika kuendesha maisha yao na ustawi wa jamii” alisema Khan.


Mashindano ya Ngalawa yamekuwa yakifanyika kila mwaka katika kijiiji cha Kigombe kilichopo  mpakani  mwa  wilaya Muheza na Pangani na hushirikisha vikundi mbalimbali vya ngoma za jadi pia.


“Tunaishukuru kampuni ya Zantel kwa kutusaidia kufanikisha mashindano haya kwani tunalenga kukuza mchezo wa kuendesha Ngalawa, tunaamnini kupitia mashindano hayo serikali inaweza kuongeza orodha ya mchezo huo katika mashindano ya Olimpiki” alisema mshindi wa shindano hilo Juma Mgeni.

Related

Sticky 8453270813179457972

Post a Comment

emo-but-icon

item