Matic amsifia Mourinho


KIUNGO wa Chelsea, Nemanja Matic amesifia uwezo wa kocha Jose Mourinho katika kufunidsha na kuwa chanzo cha ushindi wa 1-0 dhidi ya Manchester City, mchezo uliochezwa Etihad Stadium.

Matic alisema kuwa Mourinho ni kocha wa aina yake kwa kuwa ameiwezesha timu hiyo kupanda kwa pointi na kuwa na pointi sawa na Manchester City huku ikiwa nyuma ya Arsenal kwa pointi mbili.

Matic alisema kuwa kwa sasa anajisikia ni mwenye furaha kutokana na mafanikio hayo muhimu kwa timu yake hiyo.

"Ninayo kila sababu ya kumsifia kocha wangu huyu kutokana na mafniko yake haya kwenye timu hii ambayo leo tunaweza kutembea kwa kujiamini zaidi ingawaje tunayo kazi kubwa mbele yetu"alisema Matic.

Alisema kuwa siri kubwa  ya ushindi ni kwamba kocha aliwaonesha Video ya namna ambavyo timu hiyo ya Manchester ilivyokuwa ikicheza na kisha kujipanga namna ya kuikabili.

Alisema kuwa walijipanga na kuhakikisha kuwa mchezo huo kwao unakuwa wa ushindi na walipofuata mbinu za Mourinho kila kitu kilikuwa sawa kwao.

Alisema kuwa kwa sasa wakikutana na timu nyingine yenye uwezo na spidi sawa na Manchester City wanaweza kuikabili kwa hali na mali.


Related

Michezo 3356174564391163635

Post a Comment

emo-but-icon

item