Bayern Munich yaikomalia UEFA

MWENYEKITI wa klabu ya Bayern Munich Karl-Heinz Rummenigge amelitaka Shirikisho la Mpira wa Miguu la Ulaya (UEFA) kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya timu ya Paris Saint-Germain kwa kukiuka taratibu za usawa katika matumiz ya fedha.

Mwenyekiti huyo alipaza sauti kulalamikia matumizi hayo mabaya yaliyofayw ana timu hiyi ambayo alidai kuw ayamekiuka makubaliano ya usajili kama yanayohidhinishwa na UEFA.

Alimtaka Raisi wa UEFA Michel Platini kuiadhibu timu hiyo ambayo alisema kuwa imekiuka taratibu sahihi za usajili.

Alisema kuwa klabu hiyo imezidisha matumizi kulingana na utaratibu husika na kuongeza kuwa inafahamika kuwa chanzo chake cha kikubwa kinatoka Qatar kuwa ni bilioni 400 kwa msimu"alisema Mwenyekiti huyo.
Alimtaka Platini kulichukulia suala hilo kwa uzito wa hali ya juu hasa ikizingatiwa kuwa zipo adhabu zinazotolewa kwa klabu zinazokiuka utaratibu uliowekwa kwenye suala zima la matumizi ya fedha kwa msimu.

Alisema kuwa inatakiwa taratibu hizo zinazozibana timu katika matumizi ya ligi zisivurugwe hasa kutoka kwa matajili wa Saudi Arabia au Urusi ambao wanaonekana kuitawala zaidi ligi ya Ulaya.

Alisema kuwa ligi ya Bundesliga ni moja kati ya ligi ambazo zinafuata utaratibu huo wa UEFA na hivyo ndio sababu ya kuwa hata timu za Ufaransa zinatakiwa kufanya.

Alisema kuwa iwapo timu za nchi nyingine zisipofuata hilo basi hata za Ujerumani nazio zinaweza kujiunga pamoja nazo kukiuka taratibu hiyo.
Kwa mujibu wa kampuni inayojishughulisha ufutiliaji wa masuala ya fedha imethibitisha kuwa PSG imepata mapato ya zaidi ya bilioni 700 kwa msimu wa 2012 na 2013.
==============================

Related

Michezo 1423731667098558264

Post a Comment

emo-but-icon

item