Beckham arejea tena US kuwa na timu yake
http://habari5.blogspot.com/2014/02/beckham-arejea-tena-us-kuwa-na-timu-yake.html
|
MCHEZAJI mkongwe wa soka ambae kwa sasa amestaafu fani hiyo,David Beckham kwa sasa amejipanga kurejea kwenye timu yake ya MLS franchise ya Miami nchini Marekani akiwa kama mmiliki wa timu.
Mchezaji huyo alianza kuchezea timu za Manchester United, Real Madrid, LA Galaxy, AC Milan na Paris Saint-Germain wakati wake wakicheza soka.
Beckham amedumu kwenye medani ya soka kwa miaka 20 sasa kabla ya kujihudhuru rasmi katika msimu wa mwaka 2012 na 2013.
Kwa sasa Beckham anaungana na timu yake hiyo akiiongoza kwenye ligi kuu itakayoshiriki ligi kuu Marekani mwaka 2016.
Beckham alijiunga na timu ya LA Galaxy ta Marekani mwaka 2007 akitokea Real Madrid ambapo alichezea kwa miaka minne.
|