Mtoto wa Paul Walker kurithi mali za baba yake

ALIYEKUWA mcheza filamu mahiri wa Marekani, Paul Walker amemwachia mtoto wake wa kike kitita cha shilingi bilioni 50.

Mwigizaji huyo alipoteza maisha mwaka jana  kufuatia ajali mbaya ya gari na alikuwa na mtoto huyo mmoja wa kike ambae ndio kwa sasa anarithi mali za baba yake huyo.


Mbali na kuacha urithi huo pia ameacha nyumba ya thamani ya bilioni 20 ambayo nayo inachukuliwa na mwanawe huyo.


Kwa mujibu wa nakala iliyotolewa katika mahakama ya Santa Barbara iliyopo  California ilielezakuwa Walker aliwahi kuandika wosia huo ambao aliweka wazi kila kitu.

Katika walaka huo Walker alimchagua baba yake mzazi aitwae Paul kusimamia kila kitu chake huku mama yake mzazi aitwae Cheryl kuwa kama mlezi wa binti yake huyo aliezaa na mpenzi wake wa awali Rebecca McBrain.


Nakala hizo aliandika mwaka 2001 wakati alipoanza kuigiza filamu yake ya kwanza ya The Fast and the Furious lakini wkaati huo huo alikuwa ameshaanza kuigiza filamu kama vile Varsity Blues na She's All That.

Inasemekana kuwa binti yake huyo aitwae, Meadow alikulia zaidi kwa mama yake lakini alihamia California miaka miwili iliyopita na kuishi na baba yake.
===============================

Related

Sticky 8085267479458249732

Post a Comment

emo-but-icon

item