Mariah Carrey na mumewe Nick wanauza jumba lao
http://habari5.blogspot.com/2014/02/mariah-carrey-na-mumewe-nick-wanauza.html
Mariah na Serengeti wake |
Kitanda hapa ni moja kati ya vyumba vilivyopo jumbani humo |
Jumba hilo kwa mbele |
Ndani ya Jumba hilo |
Jumba hilo la kifahari wanaliuza kwa dola za kimarekani milioni 13 fedha ambazo ni mara mbili ya zile walizotumia kununua Jumba hiyo.
Jumba hilo walilinunua kwa dola milioni 7 mwaka 2009 muda tu baada ya kufunga ndoa.
Watoto wao wawili ambao ni mapacha Moroccan na Monroe walizaliwa wakiwa kwenye jumba hilo ambalo kwa sasa wanaliuza.
Lina ukubwa kwa meta 11,750, vyumba mabafu tisa pamoja na vitu vingine vya thamani.
Lina sehemu ya kuegeshea magari zaidi ya 20, ukumbi wa sinema, ukumbi wa kufanyia sherehe mbalimbali yenye kuchukua watu zaidi ya 100.
Maria Carey ambae mara kwa mara katika shoo zake amekuwa akiwa na masharti mengi kuhusiana na vitu anavyotaka viwekwe kweny chumba chake cha kubadilishia nguo.
Kutangaza kuuzwa kwa nyumba yao hiyo kumevuta hisia za watu mbalimbali Marekani ambao wamekuwa wakitaka kufahamu ni jumba gani jingine ambao wapenzi hao watalinunua.